Wachimbaji wadogo Mkalama kupewa leseni zilizohodhiwa na wageni- Biteko
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waziri wa Wizara ya Madini, Doto Biteko akiwasilisha salamu za Wizara hiyo kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika hii leo katika viwanja vya Halmashauri ya Mkalama mkoani Singida ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani humo iliyoanza Februari 16, 2019.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Wizara ya Madini, Doto Biteko akiwasilisha salamu za Wizara hiyo kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (wa kwanza kushoto) katika Halmashauri ya Mkalama mkoani Singida.
Waziri wa
Madini, Doto Biteko amesema wizara hiyo inatarajia kuzifuta leseni 38 za
utafiti wa madini zinazoshikiliwa bila kuendelezwa na wawekezaji wa kigeni
katika Wilaya ya Mkalama mkoani Singida na kisha kuzigawa upya kwa wachimbaji
wadogo.
Waziri
Biteko ameyasema hayo leo wakati akitoa salamu zake kwenye mkutano wa hadhara
wa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, alioufanya katika eneo la Nduguti
ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kikazi mkoani Singida aliyoianza Februari
16, 2019.
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments: