LIVE STREAM ADS

Header Ads

Alichozungumza Mkuu wa Mkoa Mwanza kwenye maadhimisho ya miaka 42 ya CCM

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Februari 03, 2019 kimeadhimisha kumbukizi ya miaka 42 tangua kuasisiwa kwake Februari 05, 1977. Maadhimisho hayo yamefanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Buhongwa na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu wa CCM Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu, Ngemela Lubinga.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza ambaye pia ni Mjumbe Kamati ya Siasa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto), na Katibu wa CCM Mkoa Mwanza, Adam Ngalawa (kulia), wakipanda mche katika Shule ya Msingi Buhongwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 42 tangu kuzaliwa CCM.
Maadhimisho ya miaka 42 ya Chama cha Mapinduzi wilayani Nyamagana yameungwa mkono na wilaya zote mkoani Mwanza ambapo shughuli mbalimbali za kijamii zimefanyika ikiwemo kukabidhi zawadi kwa watoto yatima katika Kituo cha SOS Igeregere Mahina, kushiriki usafi katika soko na Zahanati ya Buhongwa pamoja na mgeni rasmi kuweka jiwe la msingi ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Lwanhima.
Mgeni rasmi, Katibu wa CCM Siana na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (wa pili kushoto), akimlisha keki Katibu wa CCM Mkoa Mwanza, Adam Ngalawa (wa pili kulia) kwenye maadhimisho ya miaka 42 tangu kuzaliwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, 
Katibu wa CCM Mkoa Mwanza, Adam Ngalawa (kulia), akimlisha keki Mgeni rasmi, Katibu wa CCM Siana na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga (katikati).
Katika maadhimisho hayo, Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa Mwanza, kimevuna mamia ya wanachama wapya na hapa wanakabidhiwa kadi na mgeni rasmi, Katibu wa CCM Siana na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga.
Wanachama wapya wa CCM Mkoa Mwanza wakikabidhiwa kadi na Mgeni rasmi, Katibu wa CCM Siana na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga
Mgeni rasmi, Katibu wa CCM Siana na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga akiwakabidhi kadi za CCM wanachama wapya mkoani Mwanza.
Baadhi ya wanachama wapya wa CCM mkoani Mwanza, wakila kiapo cha uaminifu.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.