LIVE STREAM ADS

Header Ads

Makamu wa Rais akagua miradi ya maendeleo mkoani Tabora

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Makamu wa Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan (pichani) jana amekagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya za Kaliua na Urambo mkoani Tabora, kabla ya kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara aliyoifanya kwa wilaya zote mbili.

Mama Samia anaendelea na ziara yake ya siku tano mkoani Tabora iliyoanza Februari 21, 2019 ambapo leo akiwa wilayani Kaliua, amekagua na kuweka jiwe la ufunguzi kwenye jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya Kaliua.

Pia alikagua na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya Kaliua na kisha kuzungumza na wananchi katika uwanja wa Kolimba. Aidha alikagua na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Kituo cha Afya Uyumbu kilichopo wilayani Urambo, kukabidhi hundi ya shilingi milioni 207 kwa vikundi vya wanawake na vijana, kukabidhi bodaboda 12 kwa vijana na baadaye kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akikabidhi hundi ya shilingi milioni 207 kwa vikundi vya wanawake na vijana zilizotolewa na Halmashauri ya wilaya ya Kaliua mkoani Tabora ikiwa ni takwa la kisheria kwamba kila Halmashauri nchini inapaswa kutoa asilimia 10 ya mapato yake kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ili kuwainua kiuchumi.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akikabidhi hundi ya shilingi milioni 207 kwa vikundi vya wanawake na vijana wilayani Kaliua.

Ujenzi wa Hospitali ya wilaya Kaliua unaendelea vyema na Serikali imeombwa kusaidia ujenzi wake ili ifunguliwe Julai mwaka huu.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, akipanda mche wa mtu baada ya kukagua na kuweka jiwe la ufunguzi kwenye jengo la mama na mtoto katika Kituo cha Afya Kaliua.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akimwagilia maji mche huo.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akiweka kumbukumbu ya picha kwenye mche alioupanda.
Vikundi mbalimbali vya wajasiriamali wilayani Kaliua.
Sehemu ya wakazi wa Kaliua waliojitokeza kumsikiliza Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Kolimba.
Wananchi waliojitokeza kumsikiliza Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan wilayani Kaliua.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan pia alikagua na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Afya Uyumbu katika wilaya ya Urambo mkoani Tabora.
Baadhi ya majengo katika Kituo cha Afya Uyumbu wilayani Urambo.
Sehemu ya majengo katika Kituo cha Afya Uyumbu wilayani Uyumbu kinachotarajiwa kufunguliwa baada ya ujenzi wake kukamilika.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akipanda mche wa mti bada ya kukagua na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Kituo cha Afya Uyumbu wilayani Urambo.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kumsikiliza Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Uyumbu.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.