LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mimi siko tayari kutumbuliwa/ aondoke yeye- Aweso

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri wa Maji, Juma Aweso ameagiza kuondolewa kazini Mhandisi wa Maji katika Halmashauri ya Wilaya Kaliua mkoani Tabora, Fikiri Samadi baada ya kushindwa kusimamia mradi wa maji katika Halmashauri hiyo.

Aweso aliyasema hayo jana wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa Makamu Rais wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan uliofanyika kwenye uwanja wa Kolimba wilayani Kaliua.

Mama Samia anaendelea na ziara yake ya siku tano mkoani Tabora iliyoanza Februari 21, 2019 ambapo leo akiwa wilayani Kaliua, amekagua na kuweka jiwe la ufunguzi kwenye jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya Kaliua.

Pia alikagua na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Wilaya Kaliua. Pia amekagua na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Kituo cha Afya Uyumbu kilichopo wilayani Urambo na baadaye kuzungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.