Wanawake migodini walia kubaguliwa wakati wa hedhi "wanasema tunazuia dhahabu"
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Joel Maduka, Geita
Suala la mfumo dume bado
limeendelea kutajwa kuwa kisababishi kikubwa kwa wanawake kubaguliwa katika
maeneo ya migodini na hivyo kusababisha wengi wao kushindwa kujikwamua
kiuchumi.
Hayo yameelezwa kwenye
mkutano wa shirika lisilo la kiserikali la Biashara na Haki za Binadamu, kwa
kushirikiana na wanawake wachimbaji wa madini mkoani Geita.
Baadhi ya wanawake
wachimbaji wa madini ya dhahabu mkoani humo wanawasema, wamekuwa wakizuiliwa
kufika kwenye mashimo ya kuchimba dhahabu wanapokuwa kwenye mzunguko wa hedhi
kwa madai kwamba wanaweza kusababisha dhahabu kutopatikana.
Mwenyekiti wa chama
cha wanawake wachimbaji dhahabu koani Geita (GEWOMA), Asia Hussein anasema
kukosekana kwa elimu kwa wanawake wengi wa maeneo ya migodi ni chanzo kinachosababisha
mfumo dume kuendelea kuwepo maeneo ya migodini.
Naye Theresia Sawale ambaye
ni mratibu wa mradi wa ushirikishaji jinsia katika masula ya madini kutoka
shirika la Biashara na Haki za Binadamu anasema shirika hilo limeanza kutoa
elimu kwa wanaume maeneo mbalimbali ikiwemo migodini ili kutambua thamani ya
mwanamke katika kujitafutia kipato hususani maeneo ya migodini.
Tazama BMG Online TV hapa chini
SOMA>>> Fursa ya viwanja wilayani Chanzo
No comments: