LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mapambano ya mimba na ndoa za utotoni yaendelea mkoani Pwani

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala akiongea na vijana kijiweni kuhusu athari za mimba na ndoa za utotoni.
Na Fredy Mgunda, PwaniMkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala akiongea na vijana kijiweni kuhusu athari za mimba na ndoa za utotoni.
Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza Mkurugenzi Mkazi wa Repssi Tanzania, Edwick Mapalala.


Shirika linalojihusisha na masuala ya kijamii na kisaikolojia kwa watoto (REPSSI), limeendelea kufanya kampeni ya kutokomeza changamoto ya ndoa na mimba za utotoni mkoani Pwani.

Kampeni hiyo inafanyika ili kuhakikisha watoto wa kike wanatimiza ndoto zao za kielimu ili kushiriki katika mkakati wa Serikali wa Tanzania ya viwanda.

Akizungumza na wakazi wa Kibiti mkoani Pwani, Mkurugenzi Mkazi wa REPPSI Tanzania, Edwick Mapalala alisema tatizo la mimba na ndoa za utotoni bado kubwa na kwamba linahitaji jitihada za pamoja kupambana nalo.

“Mfano ni hizi kampeni za kutoa elimu na kuihamasisha jamii kumthamini mtoto wa kike zinasaidia kwa hiyo kama tutaendelea nazo jamii itaelewa, watoto watatimiza ndoto zao,” alisema.

Mapalala alisema REPSSI inashirikiana na shirika la Pasada linalojihusisha na masuala ya Ukimwi chini ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam na Pwani na kwamba vijana hususani madereva bodaboda wamefikishiwa elimu kuhusu thamani ya mtoto wa kike.

Baadhi ya viongozi wa Vijiji na Kata walikiri kuwa ndoa za utotoni ni changamoto kubwa lakini wanaendelea kupambana nayo.

Mratibu wa Elimu Kata ya Salala, wilayani Kibiti Erasmus Assenga alisema kwa mwaka huu tu wanafunzi wawili wa Sekondari katika kata hiyo wameacha masomo kwa mimba.

“Kwa hiyo kampeni hii ni muhimu kwa sababu watoto wa kike wenyewe wanafikishiwa elimu, jamii hasa wanaume wanaelezwa na wanajua umuhimu wa kuwathamini,” alisisitiza.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Pasada, Ester Mbwana alisema anaamini kuwa baada ya kampeni hizo kutakuwa na mafanikio makubwa kwa sababu, jamii inaelewa na imekubali kusaidia katika ulinzi wa mtoto.

No comments:

Powered by Blogger.