LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkuu wa Mkoa Mwanza kuwa mgeni rasmi mkutani wa wanamuziki

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na Dotto Mwaibale
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela leo Februari 23, 2019 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano utakao wakutanisha wanamuziki wa fani mbalimbali waliopo jijini Mwanza ulioandaliwa na Umoja wa Wanamuzi Tanzania (TAMUFO)

Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Mwanza, Rais wa TAMUFO, Dkt.Donald Kisanga (pichani) alisema mbali ya Mongela kuwa mgeni rasmi pia kutakuwa na Mbunge wa Kiteto, Mheshimiwa Koshuma ambaye atakuwa mgeni maalumu.

Akizungumzia mkutano huo, Dk.Kisanga alisema ni wa muhimu sana kwa wanamuziki hao kwani kutakuwepo na fursa nyingi.

"Mkutano huu utakaofanyika New Mwanza Hoteli ni wa muhimu sana hivyo nawaomba wanamuzi mbalimbali kufika kwani ni fursa ya pekee". Alisema Kisanga.

Kisanga alisema mkutano huo umejaa fursa mbalimbali na kuwa TAMUFO imezialika taasisi mbalaimbali ili kuelezea fursa walizonazo ili kuboresha maisha ya wanamuziki. Alisema kwamba maandalizi yote ya mkutano huo yamekwisha kamilika.

No comments:

Powered by Blogger.