Zantel yaendelea kumwaga zawadi kwa wateja wake
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Meneja wa Zantel kitengo cha bidhaa EZYPESA Leonard Kameta (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya na washindi waliopokea zawadi zao za simu za kisasa za mkononi (SmartPhones).

Promosheni kubwa ya kampuni ya mawasiliano ya Zantel ya "Tumia EzyPesa Ushinde" ambayo imezinduliwa mapema mwezi huu, inaendelea kushika kasi ambapo watumiaji wake wengi wanaendelea kujishindia zawadi za simu za kisasa za "SmartPhone" na inawezesha pia kujishindia fedha taslimu.
Meneja wa mawasiliano wa Zantel, Rukia Mtingwa amesema promosheni hiyo itadumu kwa kipindi cha miezi mitatu na hadi kufikia sasa zimefanyika droo mbili ambazo zimewezesha wateja 60 kujishindia simu za SmartPhone na pia kutakuwepo droo ya mwezi ambayo itawezesha wateja kujishindia fedha taslimu kati ya shilingi 200,000 mpaka shilingi 1,000,000 na wateja wapya wanapatiwa motisha.
Na Cathbert Kajuna




No comments: