LIVE STREAM ADS

Header Ads

"Maafisa Habari wanapaswa kutoa taarifa muhimu kwa umma"- Wakili

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Wakili James Marenga (pichani) amesisitiza kwamba Maafisa Habari wa taasisi mbalimbali ikiwemo za Serikali, wanao wajibu wa kufahamu taarifa muhimu za taasisi zao na kuzitoa kwa umma badala ya kusubiri zitolewe na viongozi wakuu pekee.

Wakili Marenga ameyasema hayo leo, kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu yanayofanyika Mjini Bariadi yakilenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu sheria mpya za vyombo vya habari na haki ya upatikanaji taarifa 

"Kwa mujibu wa Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa, Afisa Habari kutoka taasisi yoyote anapaswa kuwa na taarifa mbalimbali zinazohusiana na taasisi yake na anawajibika kuzitoa kwa umma". Amesema Wakili Marenga.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika MISA tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Internews ambapo baadhi ya washiriki wamesema yatawasa kuimarisha utendaji wao wa kazi.
BMG Habari
Wakili James Marenga akiwasilisha mada kuhusu wajibu wa vyombo vya habari katika utetezi wa haki za binadamu.
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Wakili James Marenga wakati akiwasilisha mada kuhusu maeneo yenye changamoto katika Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 pamoja na Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ya mwaka 2016.
Wakili James Marenga akiwasilisha mada kuhusu Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016.
Mafunzo hayo yanagusia sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016, Sheria ya Haki ya Kupata Taarifa ya mwaka 2016, Sheria ya Taifa ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma za Mitandao ya Kijamii ya mwaka 2015 pamoja na Kanuni zake.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu walioshiriki mafunzo hayo.
Mafunzo hayo ya siku mbili kuanzia leo Februa 16, 2019 yanafanyika Bariadi mkoani Simiyu ikiwa ni mwendelezo wa mafunzo kwa waandishi wa habari nchini Tanzania ambayo yamekuwa yakitolewa na MISA Tanzania.
Tazama BMG Online TV haoa chini

No comments:

Powered by Blogger.