LIVE STREAM ADS

Header Ads

Baraza la Wazee wilayani Ilemela laketi kujadili mchakato wa kupata Katiba

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Judith Ferdinand, BMG
Baraza la Wazee wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, limeanza mchakato wa kuunda Katiba yake itakayotoa mwongozi wa kusimamia masuala ya wazazee ikiwemo changamoto zinazowakabili.

Akizungumza kwenye kikao cha kukusanya maoni ya kuunda Katiba hiyo, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mohamed Yusuph alisema lengo ni kukusanya maoni na mawazo yanayopendekezwa na wajumbe na kisha kuyajadili kabla ya kuwasilisha mapendekezo ya Katiba hiyo kwa Mkurugenzi wa Manispaa, John Wanga ili nae aipitie na kuwashauri kisha watampatia Mwanasheria ikishakamilika itasajiliwa rasmi.

"Katiba ya wazee itakua dira na mwongozo wa kutatua changamoto za wazee wilaya ya Ilemela ambapo katika kikao hiki kila mjumbe amepata nafasi ya kuchangia mawazo na kutoa maoni ambayo yatafanyiwa kazi kabla ya kuipeleka kwa mwanasheria na Mkurugenzi wa Halmashauri". Alisema Yusuph.

Naye Katibu wa Baraza hilo, Ndibaiyukayo Muchunguzi alisema Katiba hiyo inatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu huku baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na wajumbe yakilenga kuwa na vipengele vitakavyowawezesha kutoa huduma bora kwa wazee, kuwatatulia changamoto na wapi wapeleke matatizo yao.

Naye Diwani wa Kata ya Pasiansi, Rosemary Mayunga aliyekuwa mgeni rasmi katika kikao hicho alisema Katiba hiyo inapaswa kugusa masuala ya wazee na jamii kwa ujumla kwani baraza hilo ni chombo muhimu katika kuishauri Serikali, jamii pamoja na viongozi mbalimbali na kwamba waepuke kujiingiza kwenye masuala ya kisiasa kwani nchi inatakiwa kujengwa kwa misingi ya kizalendo.  Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.