LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Mkuu atoa miezi mitatu kwa Wakuu wa Mikoa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa (pichani) amewataka Wakuu wa Mikoa nchini hususani yenye madini, kuhakikisha wanasimamia uanzishwaji wa masoko ya madini kabla ya Juni 31, 2019.

Majaliwa alitoa agizo hilo jana wakati akifungua Soko Kuu la Madini mkoani Geita ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa Januari 22, 2019 wakati akizungumza na wadau wa madini kwamba mikoa yote nchini ianzishe masoko ya madini.

Aidha Majaliwa aliagiza viongozi wa Serikali kushirikiana vyema ikiwemo kutoa elimu kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa madini ili kutambua umuhimu wa masoko ya dhahabu na kuyatumia huku wakihakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa muda wote kwenye masoko hayo.

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila alisema masoko hayo yatasaidia kuinua soko la madini hapa nchini ambapo kwa Mkoa Geita tayari wizara hiyo imetoa leseni 18 kwa mawakala wa kununua madini pamoja na leseni 113 kwa madalali.

Naye Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel alisema huu ni wakati wa kuendelea kuijenga Geita mpya kupitia mapato ya ndani yanayotokana na fedha za mgodi na kwamba Serikali ya Mkoa huo haiko tayari kumvumilia yeyote atakayekwamisha juhudi hizo huku Mwenyekiti wa Wachimbaji Wadogo mkoani Geita, Christopher Kadio akiwasihi wachimbaji wadogo kutumia Soko Kuu la Madini mkoani Geita kuuza dhahabu zao.

Mkoa wa Geita umekuwa wa kwanza nchini kuanzisha masoko ya madini ambapo kutakuwa na masoko/ vituo madogo manane ambayo ni Lwamgasa, Nyarugusu, Katoro, Bwanga, Chato Mjini, Ushirombo, Masumbwe na Msalala huku soko kuu la madini likiwa Mjini Geita.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza kwenye ufunguzi wa Soko Kuu la Madini mkoani Geita.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akitoa salamu za wizara yake kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuzungumza na wananchi kwenye ufunguzi wa Soko Kuu la Madini mkoani Geita.
Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza kwenye ufunguzi wa Soko Kuu la Madini mkoani Geita.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akitoa taarifa ya wizara hiyo kuhusu uanzishwaji wa masoko ya madini nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akitoa salamu za mkoa huo kwenye ufunguzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela akitoa salamu kwa niaba ya umoja wa mabenki wadau wa uanzishwaji masoko ya madini nchini ambayo ni NMB, Azania na CRDB.
Banda la Tume ya Madini kutoka Wizara ya Madini.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akilakiwa na Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel wakati akiwasili mkoani humo.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia) baada ya kuwasili mkoani Geita.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James baada ya kuwasili mkoani Geita.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Tabora, Aggrey Mwanri.
Soko Kuu la Dhahabu mkoani Geita.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.