LIVE STREAM ADS

Header Ads

Pinda aongoza mkutano wa Jukwaa la Waalimu Wazalendo mkoani Iringa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwenyekiti wa Jukwa la Waalimu Wazalendo mkoani Iringa, Merysina Ngowi (kulia) akizungumza kwenye mkutano wa jukwaa hilo uliolenga kujadili masuala ya uzalendo wa wananchi wa Tanzania kwa nchi yao. Kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Mwenyekiti wa Jukwa la Waalimu Wazalendo mkoani Iringa, Merysina Ngowi (wa kwanza kushoto), akiwa na Mkuu wa Mkoa Iringa, Ally Hapi, Mkuu wa Wilaya Iringa, Richard Kasesela pamoja na Naibu Meya Manispaa Iringa, Joseph Lyata kwenye mkutano huo.
Baadhi ya waalimu wazalendo waliohudhulia mkutano huo uliongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda.
Mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.

Na Fredy Mgunda, Iringa
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda amewataka walimu mkoani Iringa kutanguliza uzalendo wa nchi yao ili kuendeleza umoja na mshikamano na amani iliyopo inayosaidia kuleta maendeleo bila kuwa na chuki na visasi ambavyo mara nyingi vimekuwa vikivuruga amani.

Akizungumza na baadhi ya walimu wa shule za sekondari na shule ya msingi mkoani Iringa, Pinda aliwataka walimu hao kujifunza nini maana ya kuwa mzalendo na ndio silaha pekee ya kuhakikisha tunakwepa kuanzisha vita kwenye nchi hii.

"Kuthamini vitu vilivyopo katika nchi yako ni moja ya kuwa mtanzania mzalendo kwa kuwa utakuwa unalinda mali za nchi na kuhakikisha amani inakuwepo kwa kuna wananchi ambao ni wazalendo na nchi yao bila kujali itikadi ya vyama vilivyopo katika nchi hiyo". Alisema Pinda.

Pinda alisema kuwa nchi nyingi ambazo hazijaingia kwenye vita ni nchi zile ambazo zimekuwa zikibadilishana uongozi bila kutumia mabavu,hivyo utaona nchi nyingi zinapigana kwa ajili ya kugombea madaraka lakini hali tofauti kwa nchi ya Tanzania.

"Angalieni nchi kama Somalia tu hapo jirani wanavyopigana kwa ajili ya kugombea kuongoza nchi huo sio uzalendo wa wananchi wa Somalia ndio maana leo hii nawaambieni kuwa lazima mjifunze nini maana ya uzalendo ili kulinda na kuthamini amani ya nchi yenu". Alisema Pinda.

Aliongeza kuwa uzalendo kwa wananchi wa Tanzania umeanza kupungua kwa kuwa watu wengi hawajui nini maana ya kuwa mazalendo hivyo wanatakiwa kujifunza katika umri huo kuwa wazalendo na nchi yao.

Aliwata walimu kuanza kuwa na uzalendo kuanzia pale ulipozaliwa au ulipokulia ndio utaanza kuijenda nchi hii kwa kuwa umeenza kuthamini toka ulipokuwa mdogo hadi ukubwani kwa kuwa watakuwa na lengo la kulinda amani ya nchi.

“Uzalendo pia huanzia pale unapohuzulia mikutano ya hadhara kwa lengo la kujifunza na kujua muelekeo wa mtaani kwako au kujua mwelekeo wa taifa kwa kuwa kwenye kila mkutano wa hadhara kuna mambo ya msingi utajifunza tu". Alisema Pinda.

Naye Mkuu wa Mkoa Iringa, Ally Hapi aliwataka walimu kuwa makini na viongozi ambao wanawachagua kwa kuwa ndio chanzo cha kuharibu maendeleo ya nchi kutokana na kiongozi huyo kutokuwa na uzalendo wa nchi yao.

Hapi aliongeza kwa kuwaambia walimu hao kuwa sehemu ya kumfundisha wananchi uzalendo ni katika umri mdogo hasa wanafunzi kwa kuwa ndio kipindi ambacho wengi wameanza kuwa na uelewa wa maisha ni nini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwa la Waalimu Wazalendo mkoani Iringa, Merysina Ngowi alimhakikishia Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda kuwa walimu wazalendo wamekuwa wazalendo kweli kweli kwa kuijenga Iringa mpya na kufanya kazi pamoja na serikali pamoja na chama tawala.

Ngowi alisema kuwa walimu wazalendo wamekuwa wakifanya kazi ya kuutangaza uzalendo kwa wanafunzi na wananchi wote ambao wanatuzunguka kwa lengo la kufanya kazi pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli

Alimuomba Pinda kufikisha salamu kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa walimu wazalendo mkoani Iringa wapo makini na wapo tayari kufanya kazi pamoja naye kwa kila jambo.

No comments:

Powered by Blogger.