LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanawake Tanzania wahimizwa kushiriki chaguzi zijazo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Manispaa ya Iringa, Ashura Jongo.

Na Fredy Mgunda, Iringa
Wanawake Manispaa ya Iringa wametakiwa kushiriki katika chaguzi mbalimbali zinazojitokeza hapa nchini ili kuongoza jamii inayowazunguka.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT), Manispaa ya Iringa, Ashura Jongo ameyasema hayo na kuongeza kuwa kuwa wanawake wanaweza kuwa viongozi wazuri tatizo ni kushindwa kuthubutu.

"Tangu mkutano wa "Beijing China" umefanikisha kutujengea uwezo wananwake kwa kupata semina mbalimbali ambazo zimetusaidia kuwa viongozi wazuri wa kuweza kuongoza kwenye kila idara hivyo mkutano ule ulitusaidia sana wanawake". Alisema Jongo.

Jongo alisema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikiwathamini wanawake kwa kuwapatia nafasi mbalimba za uongozi ambazo pia wanawake hao wamekuwa wakizitendea haki nafasi hizo.

"Nyinyi wenyewe mmekuwa mashaidi kuwa marais wetu wa awamu ya nne na serikali ya awamu ya tano mmeona jinsi gani viongozi wanawake wameongezaka katika nafasi mbalimbali za uongozi hasa kwenye nafasi za kuteuliwa na kuchaguliwa". Alisema Jongo.

Alisema kuwa ilikuwa vigumu mno kuona Rais akichagua viongozi wengi wanawake kama ilivyo hivi sasa ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameua Mawaziri wengi wanawake, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa pamoja na Wakurugenzi kutoka sekta mbalimbali kwenye serikali ya awamu ya tano.

“Mmekuwa mashahidi mkiwaona viongozi wanawake walioteuliwa na waliogombea jinsi gani wanafanya kazi sawa sawa na wanaume hivyo wanawake tutaendelea kujiamini na kuongoza vizuri kati ngazi mbalimbali ambazo tutapata nafasi ya kuongoza” alisema Jongo.

Aidha Jongo aliwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi kwa kuwa wanawake wamekuwa viongozi wazuri ila tatizo ni kushindwa kuthubutu.

"Saizi wanawake hawatakiwi kuwa na uoga wa kugombea mnatakiwa kukimbilia nafasi yeyote ili inayojitokeza kugombea kwa kuwa mnauwezo wa kuongoza na mmeonyesha kuwa mnaweza". Alisema Jongo.

Pia aliwataka wanaume kuwapa nafasi wanawake kugombea nafasi mbalimbali na kuwaondolea uoga kwa kuwa wanaweza kuongoza katika nafasi nyeti za serikali. Jongo alimalizia kwa kusema kuwa wanawake wamekuwa viongozi hata kwenye familia ndio maana familia nyingi ambazo wanawake wamepewa nafasi wamekuwa viongozi wazuri wa familia.

No comments:

Powered by Blogger.