Header Ads

Grand Finale LAKWETU CONCERT 2019 kufanyika CCM Kirumba Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na Mwandishi Maalum
Lile Tamasha kubwa la Muziki wa Injili Tanzania ambalo lina mkusanyiko wa waimbaji wa kwaya, bendi na waimbaji binafsi liitwalo Lakwetu Concert linatarajiwa kufanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Juni 02, 2019.

Mlezi wa tamasha hilo, Winfridah Gyundah anasema mwaka huu limeongezewa utamu zaidi na kwamba idadi ya vikundi shiriki imeongezeka kutoka 30 hadi 50 ndani na nje ya Mkoa Mwanza.

Anasema tamasha hilo mwaka huu limekonga nyoyo za watu wengi kwa kuzunguka makanisa mbalimbali ambapo jumla ya makanisa sita katika Wilaya za Ilemela, Nyamagana na Magu yamefikiwa.

Tamasha la Lakwetu Concert liliasisiwa mwaka 2016 ambapo hadi sasa limepokelewa vyema na hivyo kutoa fursa kwa waimbaji mbalimbali wa muziki wa injili kuonyesha vipaji vyao.

Gyundah anasema kwa mwimbaji anayetaka kushiriki katika tamasha hilo awasiliane na uongozi kupitia nambari ya simu 0767 02 84 00 kwani nafasi zipo.

No comments:

Powered by Blogger.