LIVE STREAM ADS

Header Ads

Chama cha Ushirika wa Wavuvi wilayani Chato chazinduliwa rasmi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Chato
Chama cha Ushirika wa wavuvi cha Kikumbaitale kilichopo Wilaya Chato mkoani Geita, kimezinduliwa rasmi kikiwa na lengo la kuimarisha na kuendeleza wanaushirika kimaendeleo kupitiza shughuli zao.

Katibu wa chaham hicho, Alphonce Bina anasema kilianzishwa Oktoba 22, 2018 na kusajiliwa Machi 28, 2019 kikiwa na wanachama 20 na mtaji wa shilingi 290,000 na hadi sasa mtaji umekuwa na kufikia shilingi milioni 2.45 pamoja na wanachama 49.

Bina alisema pamoja na malengo mengine, pia chama hicho kimelenga kuhamasisha na kuendelea uvuvi bora na wenye tija kwa kupinga uvuvi haramu miongoni mwa wavuvi huku akiongeza kwamba kwa sasa kinakabiliwa na changamoto za upungufu wa zana bora za uvuvi ikiwemo nyavu, mashine, majokofu na hivyo kuomba Serikali iwasaidie kutatua changamoto hizo.

Akizindua chama hicho, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega alisema ushirika huo ni wa kwanza kuundwa nchini tangu Serikali ianze kuhamasisha wavuvi kuanzisha vyama vya ushirika ambapo alishauri kijiunge na Chama cha Ushirika ngazi ya Mkoa hadi Taifa ili kuwa na nguvu ya pamoja katika kufanya maamuzi yao kimaendeleo.

Ugela alitumia fursa hiyo kukabidhi hundi ya shilingi milioni tano kwa chama hicho kwa ajili ya kukiimarisha kimtaji ambapo alitoa rai kiendelee kujiimarisha zaidi na kupata fursa ya kukopesheka kwenye taasisi za kifedha ikiwemo Benki ya Maendeleo ya Uvuvi na Kilimo Tanzania.

No comments:

Powered by Blogger.