LIVE STREAM ADS

Header Ads

Tanzania kushiriki mkutano wa kidunia wa Uwazi na Uwajibikaji (EITI) 2019

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na Edwin Soko, Paris Ufarans
Mkutano wa nane wa kidunia kuhusu uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimari za asilia ikiwemo madini, mafuta na gesi (EITI 2019), unatarajiwa kuanza kesho Juni 17 jijini Paris nchini Ufaransa.

Tanzania ni miongoni mwa nchi mbalimbali duniani zitakazoshiriki mkutano huo ili kujadili kwa pamoja mafanikio ya mkakati wa uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimari hizo ambapo tayari washiriki wa mkutano huo kutoka Tanzania wamewasili salama Ufaransa.

Washiriki kutoka Tanzania katika mkutano huo wametoka katika sekta mbalimbali zikiwemo za kiserikali, Kamati ya Uwazi na Uwajibikaji (TEITI Tanzania), asasi za kiraia pamoja na waandishi wa habari.

Kwa upande wa Serikali ya Tanzania, Waziri wa Madini, Doto Biteko ameongoza msafara kwenye ushiriki wa mkutano huo ambapo leo siku moja kabla ya kuanza kwa mkutano rasmi hapo kesho, anashiriki mkutano mdogo (side event) unaojadili nafasi ya wachimbaji wadogo katika maendeleo ya sekta ya madini na matumizi ya takwimu kwenye madini.

Aidha kwa upande wa Kamati ya TEITI Tanzania, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Utour Ludovick pamoja na baadhi ya wajumbe wamewasili tayari huku pia baadhi asasi za kiraia zilizopata nafasi ya kuhudhuria zikiwa ni pamoja na Haki Rasilimali ikiongozwa na Mratibu wake Rachel Changonja na taasasi ya kukuza utawala bora na uwazi Tanzania (ADLG) ya jijini Mwanza.

Pia shirika la kimataifa la HIVOS Kanda ya Afrika ya Mashariki linalohimiza uwazi katika mikataba (Open Contracting) na kuwajengea uwezo waandishi wa habari limewawezesha washiriki kutoka asasi za kiraia na waandishi wa habari kushiriki mkutano huo ili kupata ufahamu mzuri wa namna ya kuhimiza uwazi na uwajibikaji katika rasilimali za nchi.

Mkutano huo utadumu kwa siku mbili kuanzia kesho Julai 18 hadi 19, 2019 ukifanyika katika ukumbi wa OECD katikati ya Jiji la Parisi nchini Ufaransa ambapo huwa unafanyika kila baada ya miaka mitatu ukihusisha nchini washiriki wa mpango wa uwazi na uwajibikaji katika rasilimali asilia (EITI) na kutoa fursa ya kujadili mafanikio, changamoto pamoja na maazimio.

No comments:

Powered by Blogger.