Header Ads

Watoto na vijana wako hatarini na vitendo vya ukatili "ubakwaji umetajwa"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Imeelezwa kwamba watoto na vijana wako katika hatari kubwa ya kukumbwa na vitendo vya ukatili ikiwemo ubakaji, mimba na ndoa za utotoni hivyo wazazi na walenzi wanapaswa kuangalia upya njia sahihi za malezi kwa makundi hayo muhimu katika makuzi.

Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za watoto na wanawake (KIVULINI) la jijini Mwanza, Yassin Ally ameyasema hayo kufuatia kikao kazi cha wadau wa ukatili kilicholenga kuandaa mikakati ya kuboresha upatikanaji wa huduma rafiki za afya kwa vijana na wahanga wa ukatili.

Hatua hiyo inalenga kusaidia utekelezaji wa mradi wa “sauti yangu, haki yangu katika kupunguza mimba za umri mdogo Manispaa ya Ilemela” unaosimamiwa na shirika hilo. Aidha mradi huo pia kusaidia utekelezaji wa mpango mkakati wa kiaifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya watoto na wanawake (MTAKUWWA) kwa asilimia 50 hadi ifikapo mwaka 2021/22.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.