LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wadau Shinyanga wakutana kujadili mikakati ya kuboresha huduma za afya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Zainab Telack akifungua mkutano wa wadau wa huduma za afya ya uzazi na mtoto ili kujadili Mapendekezo ya sheria ndogo za uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto katika halmashauri zote mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Zainab Telack akizungumza katika mkutano wa wadau wa huduma za afya ya uzazi na mtoto. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya Shinyanga, Jasinta Mboneko na kulia ni Katibu Tawala Mkoa Shinyanga, Albert Msovela.
Mganga Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Dkt. Rashid Mfaume akiwasilisha mapendekezo/ rasimu ya sheria ndogo za Vijiji/ Halmashauri za uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto.
Mkuu wa Wilaya Shinyanga, Jasinta Mboneko akizungumza kwenye mkutano huo.
Mratibu wa Huduma za afya ya uzazi na mtoto Mkoa Shinyanga, Joyce Kondoro akitoa taarifa ya huduma za afya ya mama na mtoto mkoani humo.
Katibu Tawala Mkoa Shinyanga, Albert Msovela akiongoza majadiliano wakati wa mkutano huo.
Viongozi mbalimbali wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri mkoani Shinyanga wakifuatilia mkutano huo.
Wadau wa afya mkoani Shinyanga wakifuatilia mkutano huo.
Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya mkoani Shinyanga wakiwa ukumbini.
Mkutano ukiendelea.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Kishapu, Boniface Butondo akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala, Simon Berege akichangia hoja ukumbini.
Mkutano ukiendelea.
Wadau wakiwa ukumbini.
Na Kadama Malunde, Malunde 1 Blog
Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Zainab Telack amefungua mkutano wa wadau wa huduma za afya ya uzazi na mtoto kwa ajili ya kujadili Mapendekezo ya sheria ndogo za Vijiji/ Halmashauri za uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto katika halmashauri za wilaya mkoa wa Shinyanga. 

Mkutano huo uliolenga kujadili kwa pamoja mikakati inayolenga kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto ili kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga,umefanyika leo Jumatatu Juni 3,2019 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

Telack alisema ili kuondoa vifo hivyo ni vyema akina mama wajawazito wanahudhuria kliniki akibainisha kuwa pia ni jukumu la baba kumhamasisha mkewe kuhudhuria kliniki na kujifungulia kwenye vituo vya afya.

"Takwimu za mwaka 2018 zinaonesha kuwa vifo vitokanavyo na uzazi mkoani Shinyanga vilipungua hadi 56 kutoka vifo 73 mwaka 2017,vifo vya watoto wachanga vilipungua kutoka 915 mwaka 2017 hadi 913 mwaka 2018" alieleza.

"Ingawa takwimu za vifo zinaonesha kupungua.Nia ya serikali ni kuhakikisha mama mjamzito anajifungua salama na mtoto wake anakua, sote tutambue kuwa hakuna mama anayestahili kufa wakati wa uzazi wala mtoto mchanga, hivyo ni lazima wadau wote tusongeze jitihada, mikakati na rasilimali ili kuhakikisha tunakuwa na vifo sifuri”,aliongeza Telack.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema, rasimu ya mapendekezo ya uundwaji wa sheria ndogo za kuboresha afya ya uzazi na mtoto imejumuisha mawazo kutoka kwa watendaji wa sekta ya afya ngazi za halmashauri na kusititiza kuwa sheria ndogo zitakazoundwa zisikinzane na Sheria mama,sera na miongozo katika sekta ya afya.

"Ninafurahi kuona kwamba moja ya mkakati katika makubaliano yetu wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya ‘Jiongeze Tuwavushe Salama’ unatekelezwa. Nawaelekeza wanasheria wa halmashauri na Mwanasheria wa Mkoa ambao pia ni washiriki wa mkutano huu kutumia weledi wao kushauri na kuhakikisha kwamba kazi hii inakamilika kwa wakati" aliongeza.

Akiwasilisha rasimu ya sheria ndogo za Vijiji/ Halmashauri za uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto, Mganga Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Dkt. Rashid Mfaume alivitaja visababishi vinavyochangia vifo vya mama na mtoto kuwa ni kutokuhuduria kliniki kwa wakati na mfumo dume unaosababisha mwanamke kutokuwa na maamuzi.

Alisema sababu zingine kuwa ni kutokufuata ushauri unaotolewa na wataalamu,mila na desturi potofu pamoja na jamii kukosa elimu ya kutosha kuhusu dalili za hatari za mjamzito,mzazi ana watoto wachanga.

No comments:

Powered by Blogger.