Header Ads

Kuporomoka kwa maadili "wanaume ni wachache, tunawagawana"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Waandishi wa habari mkoani Mwanza wamekuwa na mtizamo tofauti kuhusu suala la malezi mabaya kwa watoto na vijana nchini Tanzania, zaidi wakiwatupia lawama wazazi na walezi kwa kushindwa kusimamia malezi na makuzi bora kwa watoto wao.

Hayo yanaelezwa kwenye mafunzo kwa baadhi ya waandishi wa habari mkoani Mwanza yaliyoandaliwa na shirika la kutetea haki za watoto na wanawake (KIVULINI) ili kuwajengea uwezo kusaidia mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia katika jamii.

Mafunzo hayo yaliyofanyika Mei 31, 2019 ni sehemu ya kusaidia utekelezaji wa mradi wa “sauti yangu, haki yangu katika kupunguza mimba za umri mdogo Manispaa ya Ilemela” unaosimamiwa na shirika la KIVULINI ambapo pamoja na mambo mengine unalenga kuboresha upatikanaji wa huduma bora na rafiki za afya kwa vijana na wahanga wa ukatili ikiwemo ubakaji na kutokomeza mimba katika umri mdogo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waandishi wa Habari mkoani Mwanza walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia mada kutoka kwa Afisa Programu wa shirika la KIVULINI, Eunice Mayengela.
Afisa Programu kutoka shirika la KIVULINI, Eunice Mayengela akiwasilisha mada kwenye mafunzo hayo ikiwemo sheria zinazomlinda mtoto nchini Tanzania.
Waandishi wa Habari mkoani Mwanza walioshiriki mafunzo hayo wakifuatilia mada mbalimbali.
Baadhi ya waandishi wa Habari mkoani Mwanza wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Mwanza walioshiriki mafunzo hayo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.