LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mongella ashuhudia Pamba SC ikilazimishwa sare na Kagera Sugar

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ameungana na mashabiki wengine wa soka kushuhudia mtanange baina ya timu ya soka ya Pamba SC dhidi ya Kagera Sugar ambapo hata hivyo mambo yamekuwa magumu baada ya timu ya nyumbani Pamba SC kulazimishwa sare tasa katika uwanja wa Nyamagana.

Kwa matokeo hayo, Kagera Sugar wamejiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kubaki Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa watashinda mchezo ujao wa nyumbani, utakaopigwa jumamosi Juni 08, 2019 katika uwanja wa  Kaitaba.

Itakumbukwa Kagera Sugar imeangukia katika michezo ya mtoano “Play Off” baada ya kumaliza katika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa mwaka 2018/19, wakati Pamba SC ilimaliza katika nafasi ya pili kwenye Kundi B katika Ligi Daraja la Kwanza hivyo inawania nafasi ya kupanda Ligi Kuu msimu ujao.

Kikosi cha Pamba SC kilikuwa; Deus Tilusubya, Hassan Kabailo, Amos Ikuzungura, Alex Joseph, John Mtobesya, Salum Ally, Yussuf Dunia, Salum Juma, Shija Mkina, Elias Seth/ Kelvin John dk 69 na Ally Rajab/ David Richard dk 84. 

Kagera Sugar; Ramadhani Chalamanda, Mwaita Gereza, David Luhende, Juma Nyosso, JUma Shemvuni, Peter Mwalyanzi, Suleiman Mangoma, Ally Ramadhani, Ramadhani Kapera, Paul Ngalyoma/Jerson Tegete dk. 68 na Venende Ludovic/ Japhet Makalai dk. 53.
Waamuzi na wachezaji wa timu ya soka ya Pamba SCwakiingia uwanjani kumenyana na timu ya Kagera Sugar kuwania nafasi ya kucheka Ligi Kuu msima ujao.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mchezo huo akipokelewa na Kamisaa wa mchezo huo kwa ajili ya kukagua timu.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akisalimiana na wachezaji wa timu ya soka ya Kagera Sugar wanacheza mechi za "Play Off" kuwania nafasi ya kubaki Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu ujao.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akisalimiana na wachezaji wa Kagera Sugar.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akisalimiana na wachezaji wa timu ya soka ya Pamba SC ya jijini Mwanza inayowania nafasi ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao ambapo kwa sasa timu hiyo iko Ligi Daraja la Kwanza.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akisalimiana na wachezaji wa timu ya Pamba SC.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella kikosi cha akiba cha timu ya Pamba SC.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akisalimiana na kikosi cha akiba cha timu ya Kagera Sugar.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akisalimiana na kikosi cha akiba cha Kagera Sugar.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akisalimiana na benchi la ufundi la Kagera Sugar.
Wadau mbalimbali wa soka jijini Mwanza wakisalimiana na wachezaji.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula ndaye alikuwepo kutoa hamasa kwa wachezaji.
Mdau wa michezo, Altaaf Mansoor "Dogo" kutoka kampuni ya MOIL naye alikuwepo kutoa hamasa kwa wachezaji.
Kikosi cha timu ya soka ya Kagera Sugar.
Kikosi cha timu ya Pamba SC ya jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akifuatilia mtanange huo. Kushoto ni Katibu Tawala mkoani Kagera, Profesa Faustine Kamuzota na kulia ni Naibu Meya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (wa pili kushoto waliokaa) pamoja na viongozi mbalimbali na mashabiki wakifuatilia mtanange dhidi ya Pamba SC na Kagera Sugar uliopigwa kwenye uwanja wa Nyamagana.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (wa pili kushoto waliokaa), viongozi na mashabiki wa soka jijini Mwanza wakifuatilia mtanange huo.
Viongozi mbalimbali mkoani Mwanza wakifuatilia mtanange baina ya Pamba SC na Kagera Sugar
Mashabiki wa soka jijini Mwanza wakifuatilia mchezo huo.
Mashabiki wa soka mkoani Mwanza wakifuatilia mtanange huo.
Mashabiki wa soka wakifuatilia mtanange huo.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (wa tatu kushoto) pamoja na mashabiki mbalimbali wakifuatilia mtanange huo.
Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, ACP. Jumanne Mliro (kushoto) naye alikuwepo uwanjani.
Mashabiki wa soka jijini Mwanza wakifuatilia mchezo huo.
Mkurugenzi wa MOIL, Altaaf Mansoor naye alikuwepo uwanjani kutoa hamasa.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (katikati), Katibu Tawala mkoani Kagera (kushoto) na Katibu wa CCM Wilaya Nyamagana, Solomon Kasaba (kulia) wakifuatilia mchezo huo.
Baada ya mchezo, mashabiki wa soka jijini Mwanza wakaweka kumbukumbu kupitia BMG.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi/ mashabiki wengine wa soka jijini Mwanza.
Mashabiki wa soka jijini Mwanza akiwemo Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula (wa pili kushoto).
#PamojaDaimaBMG

No comments:

Powered by Blogger.