LIVE STREAM ADS

Header Ads

Viongozi wapya MPC kukutana na Kamati ya Amani Mkoa Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwenyekiti mpya wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (Mwanza Press Club-MPC), Edwin Soko amekutana na viongozi wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa Mwanza wakiongozwa na Mwenyekiti Mwenza Sheikh Hassan Kabeke.

Kikao hicho cha dharura kililenga kuweka ahadi ya viongozi wapya wa MPC waliochaguliwa Juni 01, 2019 kupitia Mkutano Mkuu Maalum kukutana na Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa Mwanza ili kuweka mikakati ya kuanzisha ushirikiano baina ya taasisi zote mbili kwa mstakabali wa amani ya Mkoa Mwanza na Taifa kwa ujumla.

Baada ya majadiliano mafupi, viongozi hao wamekubaliana kukutana hivi karibuni.
#BMGHabari
Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko (kilia) akisalimiana na Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa Mwanza, Sheikh Hassan Kabeke (kushoto).
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.