Pamba SC ya Mwanza yaapa kurejea Ligi Kuu “tutapata matokeo Kagera”
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Licha ya
timu ya soka ya Pamba SC ya jijini Mwanza kulazimishwa suluhu (0-0) na Kagera Sugar
katika uwanja wa Nyamagana hapo jana Juni 03, 2019, bado timu hiyo imeleza
matumaini yake makubwa ya kupata ushindi kwenye mchezo wa marudiano jumamosi
Juni 08, 2019 katika uwanja wa Kaitaba Bukoba.
Pamba SC
imeangukia kwenye michezo ya mtoano (Play Off) baada ya kumaliza nafasi ya pili
katika nafasi ya pili kwenye kundi B katika ligi daraja la kwanza hivyo
inawania nafasi ya kupanda ligi kuu msimu ujao 2019/20 huku Kagera Suga ikisaka
nafasi ya kusalia ligi kuu baada ya kumaliza nafasi ya 18 kwenye msimu wa mwaka
2018/19.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mashabiki wa soka jijini Mwanza waliojitokeza kuipa hamasa timu yao ya Pamba SC kwenye mchezo wao na Kagera Sugar.
Mchezo huo ulisakatwa kwenye dimba la kisasa la Nyamagana.
Kikosi cha Pamba SC kilifanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Kagera Sugar bila mafanikio.
Mchezo ulikuwa wa kuvutia licha ya nyavu kuwa ngumu kuruhusu magoli kupenya.
Kagera Sugar pia walihakikisha hawaruhusu nyavu zao kutekenywa.
Kikosi cha Pamba SC kilikuwa na kazi ya ziada kuhakikisha kinapata ushindi nyumbani lakini mambo yakwa ndivyo sivyo hadi dakika 90 za mchezo huo.
Mashabiki walijitokeza kwa wingi ikizingatiwa hakukuwa na kiingilio mlangoni.
Kikosi cha Kagera Sugar kikiwa kwenye maombi kuhakikisha nyavu zao hazipapaswi.
Mchezaji wa Kagera Sugar akitoa nje ya uwanja kwa majonzi baada ya kushindwa kuzifumania nyavu mara kadhaa.
Mchezo huo ulishuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella, Meya wa Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha, Katibu Tawala mkoani Kagera, Process Faustine Kamuzora, Mbunge wa Nyamagana, Stanslaus Mabula pamoja na Katibu wa CCM Wilaya Nyamagana, Solomon Kasaba (hawako pichani).
Kosa kosa langoni mwa Pamba SC.
Kikosi cha Kagera Sugar kikisuka mashambulizi langoni mwa Pamba SC.
Kosa kosa langoni mwa Kagera Sugar.
Mashambulizi kadhaa langoni mwa Kagera Sugar yalishindwa kuzaa matunda.
Kikosi cha Pamba SC mara kadhaa kilijitahidi kuzipepesa nyavu za Kagera Sugar bila mafanikio.
Mikwaju kadhaa langoni mwa Kagera Sugar ilipaa juu mawinguni na kuzusha utani kutoka kwa mashabiki kwamba "kamati ya ufundi iko makini".
Mashambulizi langoni mwa Pamba SC pia yalishindwa kuzaa matunda mara kadhaa.
Mlinda mlango wa Kagera Sugar mara kadhaa alifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi ya vijana wa Pamba SC.
Tazama BMG Online TV hapa chini
No comments: