LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mongella atoa wiki moja ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ilemela

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella ametoa muda wa wiki moja, ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Wilaya Ilemela uwe umefikia hatua ya kupaua.

Mongella aliyasema hayo Julai 03, 2019 alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa Hospitali hiyo inayojengwa katika Kata ya Sangabuye (eneo la Kabusungu-Isanzu), ulioanza rasmii Machi 22, 2019 kwa gharama ya shilingi Bilioni 1.5.

Hatua hiyo inakuja baada ya ujenzi wa hospitali hiyo kutofikia maelekezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Suleimani Jafo aliyeelekeza kwamba hadi kufikia Juni 30, 2019 ujenzi wa Hospitali za Wilaya kote nchini uwe umefika hatua ya kupaua.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemelema, John Wanga (kulia) alipowasili kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Ilemela. Katikati ni Katibu Tawala Wilaya Ilemela, Said Kitinga.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) akisalimiana na viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya Ilemela alipowasili kukagua ijenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella (kushoto) akisalimiana na viongozi mbalimbali Manispaa ya Ilemela.
Ziara ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella kukagua majengo mbalimbali katika ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Ilemela.
Ukaguzi wa majengo mbalimbali katika ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Ilemela.
Ujenzi wa majengo haya unaenda kwa kasi baada ya kuchelewa kwa juma moja kulingana na muda uliokuwa umetolewa.
Majengo mbalimbali katika ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Ilemela.
Mkuu wa Mkoa Mwanza pia ameagiza miundombinu muhimu kama vile maji, umeme na barabara kufikishwa hospitalini hapo.
Shughuli mbalimbali zinaendelea kwa kasi.
Ukamilishaji wa majengo mbalimbali katika ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Ilemela.
Ujenzi ukiendelea kwa kasi.
Majengo mbalimbali katika ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Ilemela.
Wakazi wa Ilemela wakichapa kazi kwenye ujenzi huo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.