LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA- Biteko akutana na Wenyeviti wa Bodi zilizo chini ya Wizara ya Madini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Madini, Doto Biteko amekutana na Wenyeviti wa Bodi za taasissi zilizo chini ya wizara hiyo kupitia kikao kazi kilichofanyika jana Julai 03, 2019 jijini Mwanza.

Kikao hicho cha kwanza baina ya Waziri Biteko na Wenyeviti hao tangu wateuliwe kwenye nafasi zao, kililenga kujadiliana namna ya kuboresha utendaji kazi baina ya taasisi zote bila kuingiliana kimajukumu.

Kando ya kikao hicho, Waziri Biteko akawaeleza wanahabari kwamba majadiliano hayo yatawasaidia Wenyeviti hao kuendesha taasisi zao kwa weledi huku Wizara ya Madini ikinufaika na mchango wao kazini kwani wote wana uzoefu wa kutosha na hivyo kutimiza matarajio ya watanzania kuona wananufaika na Wizara hiyo.

Waziri Biteko pia alitumia fursa hiyo kuendelea kuwahimiza wachimbaji na wafanyabiashara wa madini kuachana na utoroshaji wa madini na badala yake wayatumie masoko ya madini yaliyoanzishwa katika maeneo mbalimbali nchini kuuzia madini yao na kwamba wanaokiuka utaratibu wataendelea kushughulikiwa kisheria.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.