Header Ads

Waziri wa Maji aokoa Milioni 250 "zilitengwa kufanya sherehe"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amezuia matumizi ya fedha kiasi cha Shilingi Milioni 250 zilizokuwa zimetengwa kutumika kwa ajili ya sherehe ya uzinduzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) na badala yake kuelekeza fedha hizo zikatekeleze mradi wa maji mkoani Mtwara.

Profesa Mbarawa ametoa zuio hilo jana Julai 03, 2019 wakazi akizungumza kwenye makabidhiano ya mradi wa maji Shilima uliopo Wilaya Kwimba mkoani Mwanza utakaoanza kutekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUASA) baada ya Mkandarasi kampuni ya “PALEMON Company Ltd” kushindwa kuutekeleza kwa wakati.

Aidha Profesa Mbarata alitumia fursa hiyo kueleza kwamba Serikali kupitia mamlaka zake za maji itawanyang’anya wakandarasi miradi ya maji 88 nchini na kutekelezwa na mamlaka zake na maji baada ya wakandarasi hao kushindwa kuitekeleza kwa wakati huku pia ikiokoa kiasi kikubwa cha fedha tofauti na ilipokuwa ikitekelezwa na wakandarasi hao.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Kwimba, Senyi Ngaga alisema Mkandarasi alikwamisha mradi huo kukamilika kwa wakati na hivyo kuishukru Wizara ya Maji kwa kuridhia asimamishwe kazi ili mradi utekelezwe na MWAUWASA.
Mwenyekiti wa Bodi ya MWAUWASA, Christopher Gachuma alisema mamlaka hiyo itatekeleza mradi huo kwa wakati kulingana na maelekezo ya Waziri wa Maji ambayo ni miezi miwili.
Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Wilaya Kwimba, Pius Boaz alisema mradi huo ukikamilika utasaidia kuondoa adha ya maji kwa wakazi 16, 675 wa Kata ya Kikubiji pamoja na wengine wa maeneo jirani.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa Mwanza, Hellen Bogohe akitoa salamu zake kwa niaba ya akina mama wilayani Kwimba ambao ni wahanga wakubwa wa kero ya maji.
Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi mbalimbali wakichimba mtaro wa kulaza mabomba ya maji kwenye mradi wa maji Shilima kama ishara ya kuanza kwa utekelezaji wa mradi huo chini ya MWAUWASA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza- MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga (katikati) pamoja na viongozi mbalimbali wilayani Kwimba.
Wakazi wa Kata ya Kikubiji wakifuatilia tukio hilo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.