Header Ads

Serikali yaziomba asasi za kiraia kuwa wadau wa miradi ya kimkakati

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Na Edwin Soko, Shinyanga
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama ameziomba asasi za kiraia kuwa mdau mkubwa kwenye mchakato wa utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano hasa ujenzi wa bomba la mafuta litokalo Hoima Uganda hadi Tanga Tanzania.

Waziri Mhagama alisema hayo Julai 03, 2019 mkoani Shinyanga kwenye ufunguzi wa warsha ya wadau kuhusu kukuza bidhaa za ndani (Local Conten) katika sekta ya uzinduaji mikoani iliyoandaliwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi na Asasi ya HakiRasilimali.

"Tunaziomba asasi za kiraia zinazofanya kazi katika eneo la mafuta na madini zikiongozwa na HakiRasilimali zitusaidie kwenye kuwaanda watanzania kunufaika na mradi huu wa bomba la mafuta ghafi" alisema Mhagama.

Naye Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Beng'i Mazana Issa alisema tayari baraza hilo limeanza kuandaa miundombinu ya kufanikisha mradi huo.

Naye Mkuu wa Mkoa Shinyanga, Zainabu Telack alisema Mkoa huo umejipanga kunufaika na fursa za bomba la mafuta litakalopita mkoani humo na kwamba kutakuwa na kituo kikubwa cha kuongeza kasi ya msukumo wa mafuta katika Wilaya Nzega na hivyo kuwaomba wadau kuendelea kuwajengea uwezo wananchi ili wachangamkie fursa zilizopo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi taasisi ya HakiRasilimali, Donald Kasongi alisema sera ya kukuza matumizi ya bidhaa za ndani (Local Conten) ni nguzo muhimu katika kulinufaisha Taifa na miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo bomba la mafuta hivyo ni vyema zikawepo sheria madhubuti za kusimamia utekelezaji wake.

No comments:

Powered by Blogger.