LIVE STREAM ADS

Header Ads

Taasisi ya Internews yatoa somo kwa asasi za kiraia na wanahabari Tanzania

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Asasi mbalimbali za kiraia hapa nchini zimeshauriwa kuimarisha mahusiano mema na waandishi wa habari, hatua itakayosaidia kurahisisha utekelezaji wa miradi inayosimamiwa na asasi hizo kupata ufanisi katika jamii.

Rai hiyo ilitolewa Julai 02, 2019 jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kutoka taasisi ya Internews, Wenceslaus Mushi kwenye warsha kuhusu nafasi ya vyombo vya habari na asasi za kiraia katika kuchochea shughuli za maendeleo.

Mushi alisema ni vyema asasi za kiraia zikaacha mazoea ya kuwaita waandishi wa habari kwenye matukio kama vile uzinduzi wa miradi na badala yake kuwa na mahusiano ya kudumu yatakayowasaidia waandishi wa habari kufahamu taasisi husika inafanya nini ili wanapoandika habari ama makala, waandike kwa weledi.

Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC), Edwin Soko alisema waandishi wa habari nao pia wana jukumu la kuhakikisha mahusiano baina yao na asasi za kiraia yanaimarika kwa kufanya kazi pamoja, kutembeleana na kushirikiana kwenye shughuli mbalimbali ndani na nje ya kazi.

Warsha hiyo ya siku moja iliratibiwa na MPC kwa ufadhili wa Internews na kuwahusisha zaidi ya washiriki 30 kutoka vyombo vya habari na taasisi mbalimbali za kiraia mkoani Mwanza.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kutoka Internews, Wenceslaus Mushi akizungumza kwenye warsha hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakimsikiliza kwa makini, Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kutoka taasisi ya Internews, Wenceslaus Mushi.
Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko akizungumza kwenye ufunguzi wa warsha hiyo.
Washiriki wa warsha hiyo wakimsikiliza Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko.
Mkurugenzi wa taasisi ya Demokrasia na Utawala Bora Tanzania (ADLG), Jimmy Luhende akichangia mada kwenye warsha hiyo.
Washiriki wakifuatilia mada kwenye warsha hiyo.
Washiriki kutoka taasisi mbalimbali wakifuatilia mada kwenye warsha hiyo.
Wanahabari mkoani Mwanza wakifuatilia mada kwenye warsha hiyo.
Warsha hiyo ilifanyika ukumbi wa Nyanza jijini Mwanza.
Washiriki kutoka taasisi mbalimbali mkoani Mwanza wakifuatilia mada kwenye warsha hiyo.
Warsha hiyo ililenga kuwajengea uwezo wanahabari na viongozi wa taasisi za kiraia mkoani Mwanza ili kuimarisha mahusiano yao katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo kwa pamoja.
Juzi Julai 01, 2019, Wenceslaus Mushi ambaye ni Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kutoka taasisi ya Internews yenye ofisi zake jijini Dar es salaam alitembelea ofisi za Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC) jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano kutoka Internews, Wenceslaus Mushi (kushoto) akiteta jambo na Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko (kulia) alipotembelea ofisi za MPC jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.