LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wakazi wa Kwimba walia na mradi wa maji "DC akiri Serikali ilimlea Mkandarasi"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wakazi wa Kijiji cha Shilima, Kata ya Kikubiji, Wilaya Kwimba mkoani Mwanza, wamelalamikia kuchelewa kukamilika kwa mradi wa maji Shilima ulioanza utekelezaji tangu mwaka 2013 na hivyo kuomba Serikali kuingilia kati ili mradi huo ukamilike haraka.

Baadhi ya wakazi wa Kijiji hicho walitoa kilio hicho jana Juni 13, 2019 mbele ya Mkuu wa Wilaya Kwimba, Senyi Ngaga (katikati juu) ambaye ameanza ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Kata zote za Wilaya hiyo.

Akijibu kilio cha wakazi hao, Ngaga amesema Serikali imechukua hatua kwa kumuondoa mkandarasi aliyekuwa anatekeleza mradi huo kampuni ya “PALEMON Company Ltd” na kuukabidhi kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA) hivyo matarajio ni kuona mradi unaanza kutoa maji ndani ya mwaka huu.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mmoja wa wakazi wa Kijiji cha Shilima akiwasilisha kero kwenye mkutano huo.
Wakazi wa Kijiji cha Shilima, Kata ya Kikubiji wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Kwimba, Senyi Ngaga (hayuko pichani) kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika jana Juni 12, 2109.
wakazi wa Kijiji cha Sangu, Kata ya Mhande wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Kwimba, Senyi Ngaga kupitia mkutano wa hadhara.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Kwimba, Upendo Malabeja akitoa ufafanuzi kwenye mkutano wa hadhara baina ya Mkuu wa Wilaya Kwimba, Senyi Ngaga na wakazi wa Kijiji cha Sangu, Kata ya Mhande uliofanyika jana Juni 12, 2019.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.