LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Senyi Ngaga awatoa hofu wakulima wa Pamba

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mkuu wa Wilaya Kwimba mkoani Mwanza, Senyi Ngaga amewatoa hofu wakulima wa zao la pamba katika Kijiji cha Shilima, Kata ya Kikubiji wilayani humo, waliolalamikia ucheleweshwaji wa zoezi la ununuzi wa pamba mbegu licha ya msimu wa ununuzi kuzinduliwa mapema mwezi Mei mwaka huu 2019.
Mkuu wa Wilaya Kwimba mkoani Mwanza, Senyi Ngaga (katikati) akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Shilima, Kata ya Kikubiji wilayani humo kupitia mkutano wa hadhara uliolenga kuwahamasisha kushiriki shughuli za maendeleo, kusikiliza na kuzitolea majibu kero zao.
Wakazi wa Kijiji cha Shilima wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Kwimba, Senyi Ngaga.
Mkuu wa Wilaya Kwimba, Senyi Ngaga (wa tatu kulia) akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wilayani Kwimba kwa ajili ya ziara ya kukagua na kuhamasisha miradi ya maendeleo.
Mradi wa ujenzi wa madarasa mawili katika Shule ya Msingi Shilima ulioanzishwa kwa nguvu za wananchi. Serikali imetoa shilingi Milioni 12 kuunga mkono juhudi za wananchi ili kumalizia ujenzi wa madarasa hayo.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.