LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC mpya Kwimba apewa majukumu mazito baada ya kuapishwa

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella amemwapisha Mkuu mpya wa wilaya ya Kwimba Mhe.Senyi Simon Ngaga na kumtaka  akatimize vyema majukumu yake ikiwemo kupambana na mauaji yatokanayo na imani za ushirikina.

Hafla ya kumwapisha Mhe. Ngaga ambaye amechukua nafasi ya Mhe. Mtemi Msafiri aliyehamishiwa Chato mkoani Geita imefanyika leo Agosti 16, 2018 katika ofisi za Mkuu wa Mkoa Mwanza.
Mkuu mpya wa wilaya ya Kwimba Mhe.Senyi Simon Ngaga (kulia), akiapa tayari kwa ajili ya kuanza kazi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella.
Mkuu mpya wa wilaya ya Kwimba Mhe.Senyi Simon Ngaga (kulia) akipokea mwongozo wa utendaji kazi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella (kushoto)
Mkuu mpya wa wilaya ya Kwimba Mhe.Senyi Simon Ngaga (kulia) akila kiapo cha maadili ya utumishi wa umma
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella akizungumza kwenye hafla hiyo
Katibu Tawala mkoani Mwanza, Christopher Kadio akiwasilisha salamu zake kwenye hafla hiyo
Mkuu mpya wa wilaya ya Kwimba Mhe.Senyi Simon Ngaga akizungumza baada ya kuapishwa
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa, Abdul Babu akitoa salamu zake kwenye hafla hiyo

No comments:

Powered by Blogger.