Mkuu wa Mkoa Mwanza azindua mpango wa uuzaji Matrekta na Zana za Kilimo
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Tazama BMG Online Tv hapo juu
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa
Mwanza Mhe.John Mongella amezindua programu ya uuzaji wa matrekta na zana za
kilimo, unaolenga kuboresha sekta ya kilimo na kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao mbalimbali.
Akizungumza
kwenye hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika jana katika ofisi za Shirika la Taifa
la Maendeleo NDC zilizopo Mkuyuni Jijini Mwanza, Mhe.Mongella aliwataka wakuu
wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri kuandaa mkakati wa kununua matrekta
hayo ili yakasaidie uzalishaji katika maeneo yao.
Mwenyekiti
wa Bodi ya NDC, Dkt.Samwel Nyantale alisema jumla ya matrekta 2,400 yanatarajiwa
kuunganishwa na kuuzwa kwa wakulima na taasisi mbalimbali nchini na kwamba utekelezaji
huo unatokana na mkopo wa dola milioni 55 kutoka serikali ya Poland kwa
serikali ya Tanzania.
Mwakilishi
wa Benki ya Kilimo Kanda ya Ziwa, Stepehen Kang’ombe alisema ili kuhakikisha progamu
hiyo inafikia malengo yaliyokusudiwa, Shirika la Taifa la Maendeleo NDC limeingia
makubaliano na benki hiyo ili kutoa mikopo ya ununuzi wa matrekta na zana za
kilimo hivyo mamlaka husika ikiwemo vyama vya ushirika ziwasaidie wakulima
kupitia vikundi vyao ili wakidhi vigezo vya kupata mikopo hiyo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella akikata utepe kuashiria uzinduzi wa program ya uuzaji matrekta na zana za kilimo mkoani Mwanza
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella akizungumza kwenye uzinduzi huo
Mkuu wa Wilaya Sengerema Mhe. Mwl. Emmanuel Kipole akiwasilisha salamu zake kwenye hafla hiyo
Mwenyekiti wa Bodi ya NDC, Dkt. Samwel Nyantale akizungumza kwenye hafla hiyo
Mwakilishi
wa Benki ya Kilimo Kanda ya Ziwa, Stepehen Kang’ombe akizungumza kwenye hafla hiyo
Tazama BMG Online Tv hapo juu
No comments: