LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA- Huduma ya maji kupatikana kama umeme wa luku

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Profesa Makame Mbarawa amezindua mpango wa kufunga mita za maji za “malipo kabla” ambapo watumiaji wa maji watakuwa wakifanya malipo kwa njia ya benki ama mitandao ya simu za rununu kabla ya kuanza hutumia huduma hiyo.

Mhe. Profesa Mbarawa alifanya uzinduzi huo jana na kubainisha kwamba mpango huo utasaidia kuondoa malalamiko ya watumiaji wa maji kubambikiziwa bili huku pia ukisaidia serikali kukusanya mapato stahiki.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Antony Sanga alisema kwa sasa huduma hiyo inatolewa kwa viongozi wa serikali na taasisi mbalimbali ikiwemo viwanda kabla ya kuwafikia wananchi wote.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Profesa Makame Mbarawa akisalimiana na wafanyakazi wa MWAUWASA

No comments:

Powered by Blogger.