Matokeo: Michuano ya Angeline Cup 2018
Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.
Judith Ferdinand, Mwanza
Timu ya soka
ya Kata ya Kirumba imeilaza timu ya Kata ya Nyamanoro kwa goli 1-0 katika mwendelezo wa mashindano ya
Angeline Jimbo Cup 2018 yanayoendelea
kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali wilayani Ilemela.
Mchezo huo uliotumua
vumbi katika uwanja wa Kona ya Bwiru ulikutanisha
timu kutoka kundi A ambapo Kirumba ilifunga goli kupitia mshambuliaji wake Boniphace
Katengasi dakika 51.
Akizungumzia
mchezo huo , diwani wa Kata ya Kirumba Alex Ngusa aliipongeza timu yake kwa
kuibuka na ushindi huo huku akisema watafanya vizuri katika mechi zijazo kwani
ndio wameanza kuwasha moto licha ya kwamba waliweza kupoteza kwenye mechi ya
kwanza ya uzinduzi baada ya kukubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya Kata ya
Ibungilo.
Ngusa alisema
wachezaji wanatakiwa kuzingatia nidhamu kwani ndio msingi wa kufanikiwa katika
soka huku akimpongeza mbunge wa jimbo lA Ilemela Angeline Mabula na kamati yake
ya maandalizi kwa kuandaa mashindano hayo maalum kwa ajili ya kuibua vipaji vya
soka kwa vijana wa jimbo hilo kama Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM)
inavyoelekeza.
Kwa upande
wake Nahodha wa timu ya Nyamanoro, Khuzaifa Ibrahim alisema wamepoteza mchezo
huo na wataenda kufanyia kazi mapungufu na makosa yaliyojitokeza ili Michezo
ijayo wafanye vizuri huku akiwaomba wapenzi wa timu hiyo waendelee kuinga mkono
na kujitokeza viwanjani kushangilia.
Hata hivyo
katika mchezo mwingine timu ya Kata ya
Ilemela ilitoa kichapo cha goli 2-1 dhidi ya Kata ya Kiseke, mchezo
uliochezwa uwanja wa Sabasaba na
kukutanisha timu kutoka kundi C.
Timu ya
Ilemela ilifunga magoli kupitia Joseph John dakika ya sita na Emanuel Samuel
dakika ya 32 huku Kiseke ikipata goli kupitia mshambuliaji wake Edwin Robert
dakika ya 12 huku katika mchezo wa tatu uliochezwa uwanja we Buswelu Kati ya timu
ya Kata ya Buswelu na Kata ya Mecco zikitoka suluhuu ya bila kufungana.
No comments: