LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkurugenzi Alliance amwomba RC Mongella kuzinusuru timu za Mwanza

Wasiliana na BMG kupitia 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com kwa huduma za Habari na Mangazo.

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe.John Mongella amezungumza na wachezaji wa timu ya Alliance FC ikiwa zimesalia siku chache kuelekea Agosti 22, 2018 ambapo msimu wa ligi kuu Tanzania Bara utaanza rasmi.

Mhe.Mongella amewapa ari kubwa wachezaji wa timu hiyo inayoshiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza katika msimu huu wa mwaka 2018/19 na kuwataka wahakikishe wanaifunga kila timu wanayokutana nayo.

Hata hivyo Mkurugenzi wa Alliance FC, James Bwire amemuomba Mhe.Mongella kuzisaidia timu za Jijini Mwanza zinazoshiriki ligi kuu kwa kuitisha kikao cha wadau wa soka pamoja na wawekezaji mbalimbali wenye fursa ya kudhamini timu hizo.

Katika mchezo wa kwanza, Alliance FC itamenyana vikali na mahasimu wao wa soka Mbao FC katika uwanja wa CCM Kirumba, Agosti 22, 2018 ambapo hadi sasa joto la mchezo huo limezidi kupanda miongoni mwa timu zote mbili pamoja na mashabiki Jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa timu ya Alliamce FC, James Bwire akizungumza baada ya Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella kuitembelea timu hiyo
Mwenyekiti Kamati ya Mashindano timu ya Alliance DC, Yusuph Budodi akiwasilisha salamu zake
Baadhi wa wachezaji wa Alliance FC
Tazama BMG Online Tv hapa chini 

No comments:

Powered by Blogger.