LIVE STREAM ADS

Header Ads

TCRA yakutana na wadau wa Mawasiliano Kanda ya Ziwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Na Judith Ferdinand #BMGHabari
Viongozi wa dini nchini wamehimizwa kuwaelimisha waumini wao kuhusu umuhimu wa kusajili laini za simu kwa alama za vidole.

Rai hiyo imetolewa leo Juni 13, 2019 na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa, Francis Mihayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya mawasiliano Kanda ya Ziwa uliolenga kusikiliza kero, kupokea maoni na mapendekezo juu ya utendaji kazi wa mamlaka hiyo uliofanyika jijini Mwanza.

"TCRA tunaendelea kusimamia sekta ya mawasiliano kwa kuanza zoezi la usajili wa laini za simu kwa mfumo wa alama za vidole (Biometria) kwa kutumia kitambulisho cha Taifa, tukiwa na nia njema ya kuhakikisha tunadhibiti na kuondoa vitendo vya uhalifu kwa njia ya mitandao hivyo wito wangu kwenu viongozi wa dini ni kutoa elimu kwa waumini wenu juu ya umuhimu wa zoezi hili.

"Tunaamini kuwa pindi tutakapo maliza zoezi hili matatizo na changamoto za udanganyifu,utapeli mitandaoni litakwisha,pia zoezi hili litakamilika desemba 31 mwaka 2019" alisema Mhandisi Mihayo.

Kwa upande wake Meneja Huduma kwa Wateja wa Tigo Kanda ya Ziwa, Beatrice Kinabo alisema ili kukamilisha zoezi la usajili wa laini kwa mfumo wa alama za vidole, ni vyema pia viongozi wa dini wakaruhusu kampuni za mitandao ya simu kuingia kwenye nyumba za ibada kwa ajili ya kuwasajili waumini wao baada ya ibada kwani siyo watu wote wanaweza kufika katika maduka ya makampuni hayo.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa sekta ya mawasiliano Kanda ya Ziwa uliofanyika jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.