LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mongella azindua wodi za kisasa katika Hospitali ya Rufaa Bugando

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amezindua wodi za kisasa za wagonjwa mashuhuri (VIP) pamoja na binafsi (Private) katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Ziwa Bugando baada ya wodi hizo kufanyiwa maboresho makubwa.

Uzinduzi huo ulifanyika Agosti 30, 2019 ambapo wodi hizo zilizokarabatiwa kwa zaidi ya shilingi milioni mia tatu zitakuwa na huduma mbalimbali ikiwemo mgonjwa kuonwa na daktari bingwa muda wowote atakapohitajika, wavuti (Internet), friji, kiyoyoji, luninga, maji ya moto na nyinginezo nyingi.
#BMGHabari
 Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Hospitali ya Rufaa Bugando, Renatus Nkwande (kulia) akiongoza sala ya maombi kabla ya uzinduzi wa wodi hizo. Katikati ni Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Hospitali ya Bugando, Profesa Abel Makubi.
 Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Monngella akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa wodi hizo.
 Uzinduzi wa wodi hizo uliambatana na zoezi la wananchi na viongozi mbalimbali kupata huduma ya upimaji bure.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.