LIVE STREAM ADS

Header Ads

Timu ya soka Alliance yatambulisha wadhamini wake

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya timu ya Alliance, Yusuph Budodi (aliyesimama) akiwatambulisha wadhamini waliojitokeza kuidhamini timu hiyo kwa msimu wa mwaka huu 2019/20.
Picha zote na Jamson Michael
Afisa Habari wa Emirate Aluminium Profile, Issa Maeda akizungumzia udhamini wao kwa timu ya Alliance FC.
Afisa Masoko Mwandamizi wa Benki ya Access, Simon Malosha akizungumzia udhamini wa benki hiyo kwa timu ya Alliance FC.
Meneja Masoko wa Mwanza Pure Drinking Water, Upendo Mhoka akizungumzia udhamini wa kampuni hiyo kwa timu ya Alliance FC.
Wanahabari.

Judith Ferdinand, BMG
Jumla ya makampuni manne yamejitokeza kuidhamini timu ya soka ya Alliance Football Club ya jijini Mwanza kwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/20 kwa udhamini wa zaidi ya shilingi milioni 400.

Akiwatambulisha wadhamini hao jana mbele ya waandishi wa habari jiiini Mwanza, Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya timu ya Alliance, Yusuph Budodi aliwataka kuwa ni Access Bank, Alliance Schools, Mwanza Pure Drinking Water pamoja na Emirate Aluminum Profile.

Baada ya utambulisho huo, Afisa Mahusiano wa kampuni ya Emirate Aluminum Profile, Issa Maeda alisema wanaamini wapo sehemu sahihi na hivyo kuitaka timu hiyo kutoa ushirikiano ili kufikia malengo

Alisema kampuni hiyo itasaidia timu hiyo katika masuala ya usafiri kama kuwezesha upatikanji wa mafuta, kutoa hamasa kwa wachezaji ambapo kampuni hiyo itakuwa inatoa zawadi ya shilingi laki tatu kwa mchezaji bora wa timu hiyo kila mwezi.

Afisa Masoko Mwandamizi wa Benki ya Access, Simon Malosha alisema benki hiyo imetoa udhamini sehemu sahihi na salama wakiwamini kwamba timu ya Alliance itaendelea kufanya vyema katika soka nchini.

Kwa upande wake Meneja Masoko wa kampuni ya maji ya "Mwanza Pure Drinking Water", Upendo Mhoka alisema kampuni hiyo ilianza kuidhamini timu ya Alliance tangu msimu uliopita hiyo ni fursa nyingine kuidhamini kwa mara ya pili ambapo matarajio ni pande zote kunufaika zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.