LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri wa Nishati amtumbua hadharani Meneja wa TANESCO

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akitoa maelekezo kwa Mwakilishi wa kampuni ya White City Guangdong JV inayosambaza umeme wa REAIII katika Wilaya ya Bukombe mkoani Geita, kuhakikisha anagawa bure vifaa vya Umeme Tayari (UMETA) kwa wananchi wenye nyumba ambazo hazihitaji kufungwa waya (wiring).
#BMGHabari
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia) akimkabidhi mmoja wa akina mama wilayani Bukombe kifaa cha UMETA kwa ajili ya kufungiwa kwenye nyumba yake.
 Mmoja wa akina mama wilayani Bukombe akimshukru Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani baada ya kutoa ahadi ya vifaa 50 vya UMETA.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (wa tatu) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa zoezi la kuwasha umeme katika Kijiji cha Kapela Kata ya Igulwa wilayani Bukombe.
 Moja ya nyumba iliyowashwa umeme katika Kijiji cha Kapela wilayani Bukombe.
 Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini akitoa salamu zake kwenye mkutano wa hadhara wa Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayuko pichani) uliofanyika katika Kijiji cha Kapela Kata ya Igulwa jimboni huo.
Mkuu wa Wilaya Bukombe, Said Nkumba akitoa salamu za Serikali kwenye mkutano huo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kulia) pamoja na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Doto Biteko ambaye pia ni Waziri wa Madini wakimsikiliza Mwakilishi wa kampuni ya White City Guangdong JV (katikati) inayosambaza umeme wa REA wilayani Bukombe.
 Baadhi ya wakazi wa Kata ya Igulwa wakifuatilia mkutano huo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), kumsimamisha kazi Meneja wa shirika hilo Wilaya Bukombe mkoani Geita kutokana na utendaji kazi usioridhisha.

Dkt. Kalemani ametoa agizo hilo Septemba 14, 2019 wakati akizungumza na wananchi kupitia mkutano wa hadhara, uliofanyika katika Kijiji cha Kapela, Kata ya Igulwa wilayani Bukombe kufuatia ziara yake ya siku moja ya kukagua maendeleo ya mradi wa kusambaza umeme vijijini (REA) awamu ya tatu.
Tazama BMG Online TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.