LIVE STREAM ADS

Header Ads

Benki ya Access yafungua milango kwa wajasiriamali na wafanyabiashara

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Uongozi wa Benki ya Access (Access Bank) umekutana na kuwajengea uwezo wa kibiashara wateja wake wapatao 300 ambao wakiwemo wajasiriamali pamoja na wafanyabiashara wadogo jijini Mwanza..

Warsha hiyo ilifanyika Septemba 14, 2019 ikihusisha washiriki kutoka maeneo mbalimbali mkoani Mwanza waliojengewa uwezo kuhusu masuala ya kifedha ikiwemo mbinu za utunzaji fedha, namna ya kukuza mtaji na kushirikiana ili kukua pamoja kibiashara.

Akifungua warsha hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza John Mongella, Mkuu wa Wilaya Nyamagana Dkt. Philis Nyimbi alisema Serikali inaendelea kuwawekea mazingira rafiki wajasiriamali na wafanyabiashara ili kufanya biashara zao.

"Tunatambua mchango wenu katika kukuza uchumi wa Mkoa wetu na nchi kwa ujumla, Serikali ya awamu ya tano ipo bega kwa bega na nyinyi ili kuhakikisha mnapata maendeleo" alisema Dkt. Nyimbi.

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mkuu Benki ya Access ambaye pia ni Mkuu wa idara ya fedha wa benki hiyo, Julius Ruwaichi aliwahimiza wajasiriamali na wafanyabiashara nchini kuendelea kunufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki hiyo ikiwemo mikopo yenye riba nafuu huku wakirejesha kwa wakati ili waendelee kukopa zaidi.

"Nawaasa endeleeni kutumia benki yenu ya Access kwa kuwa ndiyo benki inayowapa wajasiriamali mikopo kwa wingi, kumbukeni kuwa mabalozi wazuri kwa wenzenu nao waje kupata huduma" alisisitiza Ruwaichi.
#BMGHabari
Washiriki wa warsha hiyo wakimsikiliza Naibu Mkurugenzi Mkuu Benki ya Access ambaye pia ni Mkuu wa idara ya fedha wa benki hiyo, Julius Ruwaichi.
Naibu Mkurugenzi Mkuu Benki ya Access ambaye pia ni Mkuu wa idara ya fedha wa benki hiyo, Julius Ruwaichi akizungumza kwenye warsha hiyo.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi akifungua warsha hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.
Wanahabari wakinasa matukio wakati Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi akifungua warsha hiyo.


KONGAMANO LA WAFANYABIASHARA JIJINI MWANZA 
HOTUBA YA MHESHIMIWA JOHN MONGELLA (MKUU WA MKOA) MWANZA – 14/09/2019
Belmont Fairmount Hotel 

Mkuu Idara ya Fedha naMakamu Mkurugenzi Mkuu –Ndugu Julius Ruwaich
Mkuu Idara ya Biashara – Ndugu Prosper William
Mkuu Idara ya huduma za kibenki Tanzania - Michael Fraterne
Meneja waKanda ya ziwa– Emmanuel Venance
Mkufunzi namwakilishi kutoka Benki ya uwekezaji ya Ulaya – Erick Chrispin,
Viongozi kutoka taasisi mbalimbali hapa Mwanza,
Wafanya biashara wote,
Wageni waalikwa,
Mabibi na Mabwana,
Habari za Asubuhi

1. Kwanza kabisa nichukue nafasi hii ya pekee kutoa shukranizangu za dhatikwauongozi wote wa AccessBank Tanzania kwa kunialika kuwa mgeni rasmi katika kongamano hili la wafanyabisharahapa jijini Mwanza.

2. Natambua kuwa hii ni heshima kubwa sanammenipamimi kama mkuu wenu wa mkoa wa Mwanza ili kufungua kongamano hilila aina yake ambalolinajumuisha wateja na wasio wateja wa AccessBank hapa Mwanza.

3. Lakini kabla ya kufanya shughuli ya ufunguziwa kongomano,napenda kuchukua fursa ya kuwapongezawanahisa wa AccessBank kwa uamuziwenu wa kuanzisha benki ya Access hapa Tanzania na hususani jijini Mwanza ambapomlikuja hapa mwaka 2013. Natambuawanahisahaonimakampunimakubwatu ya kimataifa yenye mlengo wa kuisaidia Jamii ya kitanzaniakuondokana na umaskini kupitia sekta hii ya kifedha.Makampuni haya ni AccessHolding ya Ujerumani, KFW,IFC ,Benki ya Maendeleo ya Afrika na Microvest. Hongereni sana.

4. Pia napenda kuwapongeza, AccessBank kwa kuwa miongoni mwa taasisi za kifedha zinazokua na kufanya vizuri hapa nchini Tanzania. AccessBank wamekuamiongonimwa taasisi za kifedha nchini zinazofanyavizurinakuwawezesha watanzania kujipatia huduma za kibenki zilizo bora, rahisi na zinazopatikana kwa muda mfupi bila mlolongo mrefukwa mteja.

5. NimeambiwakwambaAccesBankmmekuwanautaratibu wa semina kama hizi katika maeneo mbalimbali nchini, niwapongeze kwani kupitia semina na makongamano kama haya watanzaniawengiwanafaidika na kutokana na elimubora ya kifedha mnayowapatia. Jamboambalolinaonyeshakuungamkonojuhudi za MuheshimiwaRais John Pombe Magufuli na serikali yake ya awamu ya tano katika kuijenga Tanzania ya viwanda, kwani miongonimwawafanyabisharahawawapowanaomilikiviwanda mbalimbali na kupitia Elimu hii basi uzalishajiutaongezeka kwa namna moja au nyingine.

6. Wafanyabiashaarawa Mwanza ni watu makinisanandiomaanawaliposikia au kupokeamwalikohuuwamejitokeza kwa wingi na kama mnavyoonahawajaniangushakiukwelimimi mkuu wao wa mkoa. Nawapongezasanana ninaombamjipigiemakofi.

7. ACCESSBANK TANZANIA imeweka mkazo na sera maalumu katika kutoa mikopo ya kuendeleza wajasiriamali hapa nchini. Ninajua AccessBank licha ya huduma za ufunguajiwa Account pia wanatoa huduma bora za mikopoambapomikopohiyo ni kwa ajili ya wajasiriamaliwanaomiliki biashara pamoja na wakulima. Jambozuri kabisa ambalohatamimilimenivutia, ni kuwawezesha wakulima hasammojammoja kwa kuwapatiamikopo kwa mashartinafuusanandiomaanawakazi wa Mbeya waliipokea taasisi hii kwa furaha kabisa.

8. Pia nafahamukuwa tangu AccessBank ianze kutoa huduma zakehapa jijini Mwanza mwaka 2013inajumla ya wateja zaidi ya 5000 wa akaunti,na pia.

· Imetoamikopo ya biashara zaidi ya 15,000 kwa wajasiriamali, yenyejumla ya shilingi zaidi ya bilioni35Ni Kiwango kikubwasanakulinganisha na muda ambao benki hii ipo hapa Mwanza.

· Pia katika kukuza sekta ya kilimo AccessBank niwapongezemaana mpaka sasa mmekwishatoamikopo ya kilimo zaidi ya 4000 yenye thamani ya shilingi zaidi ya bilioni 7.

· Kwa upande wa ajira, AccessBank hapa Mwanza niwapongezemaana mpaka sasa mmekuwawadauwakubwa katika kukuza ajira nchini. Najuamnawafanyakazizaidi ya 40 ambao nivijana tena wengiwakiwawameajiriwawakiwahawanahatauzoefu.

· Benki imekuwa ikishiriki katika kusaidia jamii katika Nyanja mbalimbali kamavile Afya, na mazingira (kwa kutoa mashuka kwa hospitali ya butimba na kushiriki zoezi la upandaji wa miti ikiwa ni hatua kubwa ya utunzajimazingira). Pia mmetoamisaada mbalimbali ya kijamii katika kusaidiavituo vya watotowanaoishi katika mazingiramagumunabadonimeambiwamnampango mwingine wa kuendeleakusaidia Jamii hii ya wanaMwanza.

9. Haya ni mafanikio makubwa kabisa ya benki na yanatia moyo kwa benki, ambayo yamepatikana katika muda wa miaka 6 tangukuingia hapa Mwanza.

10. Niwapongeze tena kwaushirikianowenu na Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) katika kufanikisha semina na kongomano hili la wafanyabishara hapa Mbeya.

11. Hivyo basi niwatakiemafunzomemakwenunyotena kwa kusema hivyonimefungua rasmi semina hii.

AccessBank – “Njia Mpya Ya Kibenki”
Asanteni sana kwa kunisikiliza.
John Mongela
Mkuu wa mkoa wa Mwanza
Tanzania.
07/09/2019

No comments:

Powered by Blogger.