LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri Jafo azipa Halmashauri mwezi mmoja

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Selemani Jafo amemwagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuandaa utaratibu wa upatikanaji wa bajeti kwa ajili ya Maafisa Maendeleo ya Jamii nchini ili kuwawezesha kutimiza majukumu yao kwa ufanisi ikiwemo kufuatilia miradi ya vikundi vya wajasiriamali kupitia fedha za asilimia 10 zinazotolewa na Halmashauri kupitia makusanyo ya ndani.

Waziri Jafo alitoa agizo hilo Oktoba 23, 2019 jijini Dodoma wakati akifunga kongamano la Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Tanzania na kuongeza kuwa maafisa hao wana mchango mkubwa katika kuchochea maendeleo nchini hivyo lazima mazingira yao ya kazi yaboreshwe kiasi cha kuvutia wasomi wa kada nyingine kutamani kusomea kada ya Maendeleo ya Jamii.

Aidha Waziri Jafo alitoa mwezi mmoja hadi kufikia Novemba 30, 2019 Halmashauri zote nchini ziwe zimefungua akaunti maalum benki kwa ajili ya ukusanyaji wa fedha za marejesho ya vikundi vya wajasiriamali vinavyonufaika na fedha za asilimia 10 zinazotolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu hatua itakayorahisisha utoaji fedha hizo kwa vikundi vingine.

Katika hatua nyingine Waziri Jafo aliwataka Maafisa Maendeleo ya Jamii nchini kubadilika/ kujitambua na kuacha kufanya kazi kwa mazoea kwani mchango wao ni mkubwa katika kuchochea maendeleo akisema atahakikisha anaifanyia mabadiliko sekta hiyo ili iendane na hadhi yake tofauti na ilivyo sasa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kongamano hilo lililofunguliwa Oktoba 22, 2019 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (hayuko pichani) likiambatana na na uzinduzi wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (CODEPATA) pamoja na Mwongozo wa Majukumu ya Wataalam wa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Sekretarieti ya Mikoa na Serikali za Mitaa.
 Waziri wa OR- TAMISEMI, Selemani Jafo (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na Mashirika yasiyo ya Kiserikali.
 Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa OR- TAMISEMI, Selemani Jafo baada ya kufunga kongamano hilo.
 Kongamano hilo la siku mbili kuanzia Oktoba 22, 2019 linatuatiwa na Mkutano wa wanachama wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (CODEPATA) Oktoba 24, 2019 
Waziri wa OR- TAMISEMI, Selemani Jafo akipokea zawadi ya saa yenye picha yake baada ya kufunga kongamano hilo.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.