LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wanawake wapewa mbinu za kugombea na kushinda Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao, Theresia Sawaya akizungumza katika mafunzo ya uongozi kwa wanawake watia nia ya kugombea nafasi za uongozi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 kutoka Vitongoji na Vijiji kutoka baadhi ya Kata za Wilaya Kishapu mkoani Shinyanga. 

Na Kadama Malunde, Malunde 1 Blog
Mtandao wa Jinsia Tanzania "TGNP Mtandao" umetoa mafunzo ya uongozi kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu waliotia nia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, 2019 ili kuwajengea uwezo, ujasiri, mbinu na mikakati ya kuingia katika kinyang'anyiro cha uchaguzi na kushinda.

Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza Jumatano Oktoba 23,2019 kwenye ukumbi wa BM uliopo katika Kata ya Maganzo Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga na kukutanisha watia nia 65 kutoka baadhi ya Kata za Wilaya hiyo.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Theresia Sawaya ambaye ni Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao alisema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo wanawake, vijana na watu wenye ulemavu waliotia nia kugombea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa ili waweze kugombea na kushinda kwa kishindo.

"Tumekutana na watia ni kugombea nafasi za uongozi kwenye uchaguzi ili kuwafundisha kuhusu dhana za jinsia na namna zinavyotumika na athari zake katika masuala ya uongozi lakini pia kuwajengea uwezo namna ya kufanya kampeni kwenye uchaguzi,namna ya kupata rasilimali fedha na ulinzi na usalama wa wagombea" alieleza Sawaya.

Alisema kupitia mafunzo hayo wanatarajia wanawake ambao katika miaka ya nyuma wamekuwa nyuma kushiriki kwenye masuala ya uchaguzi watahamasisha na kupata ujasiri wa kugombea na kushinda katika uchaguzi na kushiriki katika ngazi mbalimbali za maamuzi.

Kwa upande wake Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao, Eva Hawa ambaye pia ni Mwezeshaji katika mafunzo hayo aliwataka wanawake watia nia kugombea kwenye Uchaguzi kuhakikisha wanawashirikisha waume zao ili kupata matokeo mazuri zaidi.

"Wanawake tunapogombea madaraka ni vyema kuwashirikisha watu wanaotuzunguka, washawishini waume zenu wawaunge mkono ikibidi muwaombe wawe makampeni meneja wenu, wataongea na wanaume wenzao ili wawape kura na mtapata ushindi mnono" alisema Juma.
Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao, Theresia Sawaya akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao, Theresia Sawaya.
Wanawake watia nia kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wakiwa kwenye mafunzo hayo. Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao, Eva Hawa ambaye pia ni Mwezeshaji akifafanua jambo kwenye mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakimsikiliza Mwanasheria kutoka TGNP Mtandao, Eva Hawa ambaye pia alikuwa Mwezeshaji. 
Diwani wa Kata ya Mwadui Luhumbo, Sarah Masinga akiwatia moyo wanawake waliotia nia kugombea nafasi za uongozi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 wilayani Kishapu.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Tituo vya Taarifa na Maarifa Wilaya Kishapu, Rahel Madundo akiwasisitiza wanawake kupendana na kuacha tabia ya kukwamishana wao kwa wao.
Mtia nia ya kugombea nafasi za uongozi kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Mary Richard Nzingula akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Mlezi wa wanawake watia nia ya kugombea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 Wilaya ya Kishapu, Suzana Makoye ambaye pia ni Diwani wa Viti Maalum Kata ya Maganzo akiwasisitiza wanawake wenzake watia nia kutokata tamaa wanapokutana na changamoto mbalimbali. 

No comments:

Powered by Blogger.