LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mkuu wa Wilaya Ilala akagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Na Azmala Said, Dar
Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es salaam, Sophia Mjema ametembelea ujenzi wa mradi wa maji uliopo Mtaa wa Kichangani, Kata ya Majohe wilayani humo ambao hadi kukamilika Oktoba 30, 2019 utagharimu zaidi ya shilingi milioni mia mbili (Tsh. 229,667,088).

Ujenzi wa mradi huo unaojengwa na kampuni ya "Sk Building and Civil Engineering" ambao mpaka sasa umekamilika kwa asilimia 95 na utakapokamilika utawasaidia wakazi wa Kata hiyo kuondokana na adha ya upatikanaji wa maji.

Akizungumza baada ya kukagua mradi huo, Mjema alisema alieleza kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi huo ambao utawasaidia wananchi wa Kata hiyo kupata maji safi na salama kwa uhakika.

"Jukumu langu ni kuja kuona maendeleo yanayofanyika ili kama kuna changamoto yoyote tuone tunafanya nini lakini nimefurahishwa sana na kazi na natumaini wananchi watapata maji mradi huu utakamilika kweli Oktoba 30 mwaka huu" alisema Mjema.

Naye Kaimu Mhandisi wa Maji, Kheri Sultani alisema kukamilika kwa mradi huo kutakwenda kumaliza changamoto ya uhaba wa maji katika eneo hilo.

"Akina mama wengi walikuwa wanapata shida ya maji hivyo mradi huu utakwenda kumtua ndoo kichwani mama" alisema.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya alitembelea daraja la Viwenge ambalo limegharimu kiasi cha shilingi milioni 60 na kuagiza Mamlaka ya Barabara Mjini na Vijijini TARURA kukamilisha shughuli katika eneo hilo kabla ya msimu wa mvua kuanza.

Mmoja wa wananchi, Zuhura Abdallah ambaye ni mkazi wa Viwege aliishukuru Serikali kwa kuwajengea daraja hilo akisema litawaondolea adha waliyokuwa wakiipata wakati wa mvua kwani lilikuwa halipitiki.

No comments:

Powered by Blogger.