LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kongamano la Wataalam wa Maendeleo Tanzania "shirika la KIVULINI latoa uzoefu"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI la jijini Mwanza, Yassin Ally akitoa uzoefu kuhusu ushirikishwaji wa makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo wanaume katika kupambana na Ukatili wa Kijinsia dhidi ya watoto na wanawake kwenye kongamano la Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Tanzania, Oktoba 23, 2019 jijini Dodoma.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye kongamano hilo lililofunguliwa Oktoba 22, 2019 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. Shirika la KIVULINI ni miongoni mwa wadau waliosaidia kufanikisha kongamano hilo.
 Kongamano hilo linafanyika katika ukumbi wa "Dodoma Convention Centre" jijini Dodoma.
 Mshiriki wa kongamano hilo, Reinfrida Mathayo kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii Bweri wilayani Musoma akichangia mada kuhusu ushirikishwaji wa wanaume katika kupambana na ukatili wa kijinsia iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally.
 Mshiriki wa kongamano hilo, Reinfrida Mathayo kutoka Chuo cha Maendeleo ya Jamii Bweri wilayani Musoma ameshauri wanaume kuendelea kushirikishwa kwenye masuala mbalimbali ya kijamii kwani mchango wao ni mkubwa badala ya kuachwa nyuma huku wanawake wakipewa nafasi zaidi.
 Mshiriki Mariam Daud kutoka Halmashauri ya Kilolo akichangia mada kwenye kongamano hilo.
 Mshiriki wa kongamano hilo, Dkt. Rashid Chikoyo kutoka wilayani Moshi akichangia mada.
 Washiriki wamesema wanawake wamekuwa wakishirikishwa zaidi kwenye masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo kupambana na Ukatili wa Kijinsia tofauti na ilivyo kwa wanaume hivyo ni wakati mwafaka wanaume nao kushirikishwa ipasavyo.
Ufunguzi wa kongamano hilo Oktoba 22, 2019 uliambatana na uzinduzi wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (CODEPATA) pamoja na Mwongozo wa majukumu ya Wataalam wa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Sekretarieti ya Mkoa na Serikali za Mitaa.
 Washiriki mbalimbali akiwemo Mathias Shimo kutoka Shirika la KIVULINI wakifuatilia kongamano hilo.
 Washiriki mbalimbali wakifuatilia kongamano hilo.
 Washiriki wakifuatilia kongamano hilo.
 Washiriki wa kongamano la Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Tanzania wakifuatalia mada mbalimbali.
 Washiriki wakifuatilia mada kwenye kongamano hilo.
 Washiriki wakimsikiliza Mkurugenzi wa KIVULINI, Yassin Ally wakati akiwasilisha mada kuhusu ushirikishwaji wa makundi mbalimbali ikiwemo wanaume katika kupambana na Ukatili wa Kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.
 Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kushoto) pamoja na Afisa wa Shirika hilo, Mathias Shimo (kulia) wakiwa kwenye Kongamano la Wataalam wa Maendeleo Tanzania lililofanyika jijini Dodoma.
 Washiriki wakifuatilia kongamano hilo.
 Washiriki wakifuatilia kongamano hilo.
 Taswira ukumbini washiriki wakiwa kwenye kongamano hilo.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.