LIVE STREAM ADS

Header Ads

Midahalo wilayani Misungwi yaibua mambo ya kushangaza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Shirika la kueteta haki za wasichana na wanawake KIVULINI limeendelea kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya Misungwi mkoani Mwanza kutekeleza kwa vitendo mpango kazi wa kitaifa wa kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) kupitia kampeni/ midahalo ya wazi ili kutoa elimu kwa jamii kuachana na aina zote za ukatili wa kijinsia.

Awamu ya pili ya kampeni hiyo ilizinduliwa Oktoba 16, 2019 katika Kata ya Koromije na kufuatiwa na Kata nyingine ikiwemo Usagara, Mbarika pamoja na Buhingo ambapo elimu inatolewa kwa wanajamii kutojihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia, kuviripoti wanapovishuhudia katika ngazi husika ikiwemo Serikali ya Kijiji, kusomesha watoto wa kike na wa kiume pamoja na wanandoa kushirikiana kwenye shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa nyumba bora baada ya mavuno.

Hata hivyo katika midahalo iliyofanyika kupitia kampeni ya awamu hii ya pili, suala la ukosefu wa maadili kwa wanafunzi limezungumzwa zaidi ambapo wazazi, walezi pamoja na mamlaka za Serikali wamehimizwa kushirikiana ili kuokoa baadhi ya wanafunzi wasio waadilifu hususani wanafunzi wa kike ambao wanajiingia kwenye vitendo vya mapenzi na mbaya zaidi kusagana wenyewe kwa wenyewe.
BMG Habari
 Kikundi Sungusungu Misungwi kikitumbuiza ngoza ya asili katika mdahalo uliofanyika Kata ya Buhingo Oktoba 21, 2019.
Kikundi cha ngoma asili kikitumbuiza.
 Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akiweka mambo sawa kwenye mdahalo uliofanyika Kata ya Buhingo.
 Taswira kwenye mdahalo huo.
 Wanafunzi kutoka Shule mbalimbali Kata ya Buhingo wakifuatilia mdahalo huo.
 Burudani ikiendelea.
 Burudani ya asili.
 Kikundi cha Sungusungu wilayani Misungwi kinasaidia kufikisha elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia kwa jamii kupitia nyimbo.
 Chapa Kazi, Siyo Mkeo.
  Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akifuatilia kwa makini mdahalo huo.
 Twasira mdahalo uliofanyika Kata ya Buhingo.
 Wanafunzi wa Shule mbalimbali za Msingi na Sekondari Kata ya Buhingo walishiriki mdahalo huo.
 Mdahalo Kata ya Buhingo wilayani Misungwi.
 Wanahabari wakinasa matukio.
Afisa Tarafa ya Inonelwa wilayani Misungwi, Glory Kaywanga akifafanua jambo kwenye mdahalo huo.
 Afisa Tarafa ya Inonelwa wilayani Misungwi, Glory Kaywanga akizungumza kwenye mdahalo huo.
 Mmoja wa akina bibi Kata ya Buhingo akitoa rai kwa jamii kuachana na imani potofu zinazochangia ukatili wa kijinsia.
Katika mdahalo uliofanyika Kata ya Buhingo, Mtendaji wa Kata hiyo aliendesha harambee fupi ili kusaidia ujenzi wa choo katika Shule ya Sekondari Buhingo.
Zaidi ya Tsh. 300,000 (shilingi laki tatu) zilipatikana kwenye harambee hiyo kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa choo katika Shule ya Sekondari Buhingo wilayani Misungwi.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.