LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ukosefu wa maadili "wanafunzi wajihusisha na vitendo vya ovyo"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

 Suala la ukosefu wa maadili na malezi bora kwa watoto limetajwa kuathiri mienendo ya baadhi ya wanafunzi katika Wilaya Misungwi mkoani Mwanza ambapo inaelezwa kwamba wamekuwa wakijihusisha na vitendo viovu vya kimapenzi.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally kufuatia midahalo mbalimbali ya kutoa elimu kwa jamii ili kupinga aina zote za ukatili wa kijinsia wilayami Misungwi.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango mkakati wa kitaifa wa kupambana na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) uliozinduliwa na Halmashauri ya Wilaya Misungwi kwa kushirikiana na Shirika la KIVULINI katika Kata ya Koromije, Oktoba 16, 201 na baadae kuendelea katika Kata zingine.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Baadhi ya wanafunzi na wajamii wilayani Misungwi wakifuatilia mdahalo wa kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika Kata ya Mbarika Ijumaa Oktoba 18, 2019.
 Pia kupitia mpango jumuishi wa ustawi wa mwanamke, watoa huduma za afya ngazi ya jamii wilayani Misungwi walikabidhiwa baiskeli ili kuwarahisisha utendaji kazi wao.
 Mmoja wa watoa huduma za afya ngazi ya jamii wilayani Misungwi akikabidhiwa baiskeli.
 Baiskeli zilizotolewa kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii wilayani Misungwi kwa ajili ya kurahisisha utoaji huduma.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.