LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri wa Afya awapa nguvu Wataalam wa Maendeleo ya Jamii

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewaagiza Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kuanzia ngazi za Halmashauri na Mikoa nchini kuikataa miradi ya mashirika ya yasiyo ya kiserikali (NG0’s) ambayo utekelezaji wake unajikita kutoa semina na si ile inayoacha alama ikiwemo ujenzi miundombinu ya kutolea huduma kama majengo.

Waziri Mwalimu ametoa agizo hilo Oktoba 22, 2019 jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la 15 la Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Tanzania lililoambatana na uzinduzi wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (CODEPATA) pamoja na Mwongozo wa majukumu ya Wataalam wa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Sekretarieti ya Mkoa na Serikali za Mitaa.

Amesema mashirika hayo yamekuwa yakifanya kazi nzuri lakini nyakati zimebadilika hivyo atayaandikia barua rasmi ili kuhakikisha kila shirika linatenga asilimia 20 ya fedha za miradi yake ili kusaidia utekelezaji wa miradi inayoacha matokeo yanayoonekana “tangible output”.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza kweny kongamano hilo.
Wanahabari wakinasa habari wakari Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akifungua kongamano hilo.
 Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Tanzania wakiwa kwenye kongamano hilo litakalofuatiwa na Mkutano wa Wataala hao.
 Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Patrick Golwike akitoa ufafanuzi mfupi kuhusiana na kongamano hilo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
 Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI la jijini Mwanza, Yassin Ally akitoa salamu kwenye mkutano huo ambapo Shirika hilo ni miongoni mwa wadau waliosaidia kufanikisha kongamano hilo.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuashiria uzinduzi wa Mwongozo wa majukumu ya Wataalam wa Maendeleo ya Jamii ngazi ya Sekretarieti ya Mkoa na Serikali za Mitaa.
  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kuashiria uzinduzi rasmi wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (CODEPATA).
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akionesha zawadi ya saa yenye picha yake aliyokabidhiwa kwenye kongamano hilo.
 Wadau wakiwa kwenye kongamano hilo.
 Baadhi ya wajumbe wa kongamano hilo wakiteta jambo.
 Baadhi ya washiriki wa kongamano hilo wakijadili jambo.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto) akijali jambo mmoja wa washiriki wa kongamano hilo.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kulia) baada ya kuwasili kwa ajili ya ufunguzi wa kongamano hilo.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali.
Tazama BMG TV ONLINE hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.