Naibu Waziri wa Nishati atoa miezi sita kwa wakandarasi
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Naibu Waziri
wa Nishati, Subira Mgalu amemtaka mkandarasi kampuni ya NIPO Group kuhakikisha ifikapo
Juni 30, 2019 awe amesambaza umeme katika Vijiji vyote vilivyopo Wilaya
Sengerema mkoani Mwanza.
Mgalu alitoa
agizo hilo Disemba 21, 2019 wakati akiwasha umeme katika Kijiji cha Kanyala Halmashauri
ya Buchosa wilayani Sengerema na kuongeza kwamba agizo hilo linapaswa
kutekelezwa pia na wakandarasi wengine kote nchini.
Aidha Mgalu
alibainisha kwamba Serikali imetenga shilingi bilioni 179 ili kutekeleza mradi
wa Ujazilizi kuanzia mwezi Januari 2020 katika mikoa tisa nchini ikiwemo Mwanza
kwa ajili ya kufikisha nishati ya umeme katika maeneo ambayo hayakupata nishati
hiyo kupitia mradi wa REA.
Tazama BMG TV hapa chini
No comments: