Sengerema ‘wavuvi kambi ya Mchangani walilia umeme’
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Wavuvi katika kambi ya Mchangani
iliyopo Halmashauri ya Buchosa Wilaya Sengerema mkoani Mwanza, wameiomba Serikali
kuwafikishiwa nishati ya umeme ili waweze kuboresha zaidi shughuli
zao za mazao ya uvuvi.
Wavuvi hao walitoa ombi hilo Disemba
21, 2019 mbele ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu aliyefanya ziara ya kukagua
miundombinu ya umeme na kuzindua nishati hiyo katika Halmashauri ya Buchosa
kupitia mradi wa umeme vijijini REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza.
Akijibu ombi la wavuvi hao, Mgalu alisema
Wizara yake itawasiliana na Wizara ya Maliasili na Utalii ili kupata mwafaka
ikiwa kambi hiyo ya Mchangani inayozungukwa na pori la msitu wa Kisiwa cha Kome
inaweza kufikishiwa nishati ya umeme.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA SOMA>>> Mkusanyiko wa Habari kuhusiana na Wavuvi
No comments: