LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Magufuli kuongoza mapokezi ya Ndege iliyokamatwa Canada

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli anatarajiwa kuongoza wananchi jijini Mwanza kwenye mapokezi ya ndege aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa imekamatwa nchini Canada.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amesema mapokezi ya ndege hiyo yatafanyika Disemba 14, 2019 katika jengo jipya la mizingo lililopo eneo la uwanja wa ndege wa Mwanza.

"Ile ndege yetu iliyokuwa imekamatwa nchini Canada sasa imeachiwa, kwa furaha na kwa niaba ya wanamwanza, Mheshimiwa Rais pale uwanja wa ndege jengo jipya atatuongoza watanzania kupokea ndege yetu ambayo imenunuliwa kwa fedha za watanzania" alisema Mongella na kuongeza;

"Nimekuja hapa kuwatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Mwanza na Mikoa jirani kujitokeza kwa wingi kuanzia saa nane kamili mchana ambapo geti litakuwa wazi" alisisitiza Mongella.

Ikumbukwe kuwa ndege hiyo ilikamatwa Novemba mwaka huu 2019 ambapo Disemba 11, 2019 Rais Magufuli akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CC) kilichofanyika jijini mWANZA alisema "ndege yetu iliyokuwa inashikiliwa nchini Canada imeachiliwa na wananchi watatangaziwa tarehe ya kuwasili ili wakaipokee na tutaipokelea hapa Mwanza".

No comments:

Powered by Blogger.