LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wakulima watakiwa kujiunga na huduma Fahari Kilimo ili kurahisisha malipo yao

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa Binagi Media Group. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama binagimediagroup@gmail.com
Benki ya CRDB imewahimiza wakulima nchini kufungua akaunti isiyo na makato maarufu kama Fahari Kilimo ili kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo kupokea malipo baada ya kuuza mazao yao kupitia vyama vya msingi vya ushirika AMCOS.

Meneja wa benki hiyo tawi la Mwanza, Jeremiah Msemo aliyasema hayo kwenye Mkutano Mkuu wa 28 wa Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza uliofanyika Januari 30, 2020 katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Butimba jijini Mwanza.

Aidha Msemo alibainisha kuwa mbali na benki ya CRDB kurahisisha mfumo wa upokeaji malipo kwa wakulima, pia inatoa huduma ya mikopo yenye riba nafuu kuanzia kwa mkulima mdogo, wa kati na mkubwa.


Nao baadhi ya wakulima kutoka vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) walitumia fursa hiyo kuomba benki ya CRDB kuendelea kusogeza karibu huduma zake kwa kuongeza mawakala hadi maeneo ya vijijini ili kuwaondolea adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za kifedha.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Mwanza, Jeremiah Msemo akizungumza kwenye mkutano huo.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Mwanza, Jeremiah Msemo (kushoto) pamoja na wafanyakazi wengine wa benki hiyo alioambatana nao wakitoa salamu kwenye mkutano huo.
Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Mwanza, Jeremiah Msemo akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza.
Wanachama wa Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza wakifuatilia mkutano huo.
Wanachama wa Vyama vya Msingi mbalimbali wakifuatilia Mkutano Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza uliofanyika jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB akiwemo Meneja wa Tawi la Mwanza, Jeremiah Msemo (wa pili kushoto) wakifuatilia mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wakiwemo wafanyakazi wa Benki ya CRDB waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia Mkutano Mkuu wa Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza uliofanyika Januari 30, 2020 katika Chuo cha Ualimu Butimba jijini Mwanza.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.